Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amezipa kongore timu za JKT Oljoro ya Arusha, Mawenzi ya Morogoro na Transit Camp ya Shinyanga kwa kufanikiwa kupanda daraja la kwanza  baada ya kufanya vema kwenye hatua ya Nne Bora (Play off) iliyofikia kikomo jana Aprili mosi, mwaka huu.

Katika salamu zake za pongezi, Rais Malinzi amezitaka timu hizo sasa kujiimarisha katika nyanja za usajili na maandalizi mengine ili kuwa timu za ushindani katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambako watashiriki kuanzia msimu mpya utakaoanza Julai, mwaka huu.

“Nichukue nafasi hii kuzipongeza timu zote ambazo zimepanda daraja kutoka Ligi Daraja la Pili na kwenda Ligi Daraja la Kwanza. Pongezi nyingi ziwaendee wanafamilia wote kuanzia viongozi, wachezaji, waamuzi walioamua mechi zao, mashabiki nakadhalika,” amesema Malinzi na kuongeza:
“Huu ni uthibitisho kuwa timu zote ziliajianda vya kutosha na kupata matokeo,naamini hata Cosmopolitan nayo ilijiandaa lakini kwa bahati mbaya pointi hazijatosha kwa msimu huu. Ni imani yangu kuwa itapambana msimu ujao na kufanikiwa.”
Hali Kadhalika Rais Malinzi alizitakia kila la kheri timu zote katika kumaliza msimu na kuanza msimu ujao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...