Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh Amos Makalla ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka mkoa wa Songwe mapema jana,jijini humo huku vifijo na nderemo za kuwasili mwenge huo vikiwa vimeshamiri,Hafla ya kuupokea Mwenge huo imefanyika Wilayani Chunya April 16,2017.Mwenge huo ukiwa mkoani Mbeya utakimbizwa katika halmashauri saba,ambapo utafanya kazi ya kukagua,kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi Bilioni 10.8
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akiupokea Mwenge wa Uhuru wilayani Chunya mkoani Mbeya sambamba na kula kiapo cha kuukimbiza mwenge huo katika halmashauri zote za mkoa  wa Mbeya.
 Baadhi ya makamanda wa jeshi la Polisi ambao pia ni miongoni Mwa wakimbiza mwenge wa Uhuru uliowasali hapo mkoani Mbeya
  Baadhi ya wanachama na Wafuasi wa Chama cha Mapindizi (CCM) sambamba na viongozi wa chama wakisherehekea mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru ulio wasili  jana April 16,2017 mkoani Mbeya na kupokelewa na mkuu wa Mkoa wa  Mbeya Mh.Amos makalla 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...