Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

Napenda kutumia nafasi hii kwanza kabisa kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kuwa mzima hadi siku hii ya leo. Ni dhahiri kwamba mmekuwa pamoja tangu nilipochaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam. 


akini pia mmekuwa bega kwa bega na mimi Meya wenu wa Jiji, katika juhudi kubwa za kulifanya jiji letu kuwa la kuvutia. Hivyo nina kila sababu ya kuwashukuru na kuwapongeza sana.

Ushirikiano ambao mnaunyesha na kuendelea kuuonyesha unanipa matumani makubwa kwamba tuko pamoja katika kuhakikisha kwamba tunaleta mabadiliko makubwa katika jiji letu na hivyo kuondokana na changamoto mbalimbali zinazo likabili jiji letu. hivyo naomba tuendelee kushirikiana na kuzidi kuniombea Meya wenu niweze kufanya kazi ambazo mmenituma katika jiji letu la Dar es Salaam.

Ni wazi mnafahamu kwamba, maendeleo ya jiji letu hajawezi kuletwa bila ya nyinyi wannachi kuonyesha ushirikiano kwa viongozi wenu ambao mmetuchagua kuanzia ngazi za Mitaa, Kata, Halmashauri pamoja na jiji.

Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa na mipango mingi mizuri ambayo imelenga kuboresha maendeleo ya wananchi wake. Miongoni mwa mambo ambayo niweka na kuendelea kusimamia ili kuhakikisha kwamba wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanapata huduma mbalimbali za kijamii kwa uhakika.

Ndugu wananch wa Jiji la Dar es Salaam.

Hivi sasa tunaingia kwenye kipindi cha sikuu ya pasaka. Tunapoungana na wenzetu Wakristo katika kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, niwaombe wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendeleza kushirikiana na vyombo vyetu vya usalama katika suala zima la uimarisha wa usalama wenu.

Vyombo vya usalama vimekuwa rafiki kwa kipindi chote jambo ambalo limefanya kupungua kwa matukio ya kiuhalifu ndani ya jiji letu.

Hivyo basi nitoe rai kwa wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam, kusherehekea siku kuu hii kwa Amani na utulivu bila kuwepo kwa vurugu zozote. Salamu zangu za upendo katika sikukuu hii ya Pasaka ziwe chachu ya kuendelea kutunza amani katika jiji letu, huku mki hakikisha kwamba kila eneo ambalo watoto wenu watashiriki kwa namna moja ama nyingine kuwe na usalama wa uhakika. Tusijenge utamaduni wakukubali matukio ya kuvunja amani kwenye siku kuu maana hizi ni sherehe sio vita.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...