D: MTU WA MISIMAMO
Baada ya kumaliza darasa la nane Tabora, alipata nafasi ya kusoma chuo kikuu cha Makerere Uganda. Alisomea ualimu na alihitimu diploma mwaka 1947. Aliporudi Tanganyika, alipata nafasi ya kazi kutoka misheni na serikalini. Serikalini kulikuwa na mshahara mkubwa na marupurupu mengi kuliko misheni lakini alikataa kufanya kazi serikalini akipinga mfumo wa tofauti kubwa ya malipo.

Misimamo yake ya kupinga sera za kikoloni ilimgharimu kwani serikali ya kikoloni ilikataa kumpa nafasi ya masomo nje ya nchi. Ni kwa utetezi tu wa rafiki yake mkubwa, Father Walsh, ndipo alipokubaliwa kwenda kusoma chuo kikuu cha Edinburgh cha Scotland Uingereza, aliposomea historia, uchumi na falsafa.

E: MTU WA KUJISHUSHA
Chuoni Edinburgh alihitimu na kupata Masters na kuwa mtanganyika mweusi wa kwanza kupata mafanikio hayo. Hata hivyo, hakupata kiburi na aliporudi, akaenda kijijini kwao Butiama ambapo alijenga kwa mikono yake mwenyewe nyumba yake ili afungie ndoa na mchumba wake Maria Magige. Alichanganya saruji na mchanga yeye mwenyewe na kufyatua matofali. Wanakijiji walimshangaa msomi kama yeye kushika tope...wasomi wa wakati huo, wengi wao darasa la nne tu lakiji walikuwa daraja la juu sana.

F: MSHAWISHI
Alijiunga na harakati za siasa chini ya TAA. TAA hakikuwa chama cha siasa moja kwa moja bali kikundi cha kudai baadhi ya haki ambazo zilikuwa za wazungu pekee. Akawashawishi wazee aliowakuta wabadili malengo na kuanzisha chama rasmi cha siasa kitakachodai uhuru kamili badala ya haki fulani pekee. Wazee wakakubali na kuanzisha TANU, Julai 7, 1954 na yeye akawa mwenyekiti. TANU ikafanikiwa kuleta uhuru, 1961.

Lakini ushawishi mkubwa kabisa katika historia yake na ya nchi ni ule wa mwaka 1958 aliposhawishi wajumbe wa TANU kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa baraza la kutunga (LEGCO). Vyama mbalimbali vilitakiwa kushiriki na chama kitakachopata wajumbe(wabunge) wengi ndicho kitakachounda serikali.

Huu ndiyo uchaguzi wa kwanza kabisa nchini na mkoloni aliweka masharti magumu kwa waafrika kupiga ili kukandamiza haki zao. Masharti hayo ni kuwepo kwa viti vitatu vitakavyoshindaniwa kwa matabaka(wazungu, waasia na waafrika) huku waafrika wakitakiwa kupiga kura zote tatu. Lengo la mkoloni lilikuwa kuhakikisha baraza la kutunga sheria linakuwa na wajumbe sawa, yaani waafrika, wazungu na wahindi. Kutokana na sharti hili, uchaguzi huu uliitwa UCHAGUZI WA KURA TATU.

Masharti mengine ya kumuwezesha mwafrika kupiga kura ni kuwa na kipato cha pauni mia nne za Uingereza kwa mwaka, pia awe na kiwango cha elimu ya darasa la 12(form four) na awe ameajiriwa katika kazi maalumu.

Masharti haya yaliwakera wazee na wanachama wa TANU. Viongozi wa makao makuu na majimboni wakapanga kuususia. 
Nyerere peke yake alitaka TANU ishiriki uchaguzi huu kwa sababu alihisi kama ingesusa, chama cha wazungu cha United Tanganyika Party(UTP) kingepata mteremko na kuzoa viti vyote na kuingia kwenye baraza la kutunga sheria huku TANU kikibaki nje. Kupitia fursa hiyo, wazungu wangetunga sheria kali zaidi za kuchelewesha uhuru kwa kisingizio kwamba waafrika hawajawa tayari kujitawala huku mfano ukiwa kususia uchaguzi. 

Nyerere aliona mbali zaidi ya wenzake ndani ya chama. 
Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Septemba 1958, TANU ikapanga kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka wa 1958 mjini Tabora kuanzia Januari 21-26, 1958 kuamua hatima ya uchaguzi.

cc. Zaka Zakazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...