THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SERENGETI BOYS YAITANDIKA BURUNDI BAO 2-0 KAITABA MJINI BUKOBA LEO


Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba imepoteza mchezo wake wa pili tena wa kirafiki baada ya kukubali kuchapwa bao 2-0 na Timu ya Serengeti Boys ya jijini Dar es salaam inayojiandaa na safari ya Gabon. Mchezo wake wa kwanza wa kirafiki walinyukwa bao 3-0 na Timu ya Vijana maarufu kwa jina la Serengeti Boys katika uwanja huo huo wa Kaitaba. 
Katika mchezo wa leo bao la kwanza lilifungwa na Issa Abdu Makamba dakika ya 36 kipindi cha kwanza jezi namba 6 mgongoni aliyelifunga kwa mpira wa adhabu (frii kiki) na kuzama moja kwa moja. Bao la pili  lilifungwa dakika za majeruhi dakika ya 89  na Ibrahim Abdallah na mtanange kumalizika kwa bao 2-0 ikiwa ni jumla ya bao 5-0 ikiwa ni jumla ya mchezo wa kwanza na wa pili. Serengeti sasa baada ya kuvuna ushindi huo mkubwa wanapanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na Timu ya U-17 ya Ghana Jumatatu mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.

Wachezaji wa Timu ya Serengeti Boys wakimpongeza mfungaji wao wa bao la pili Ibrahim AbdallahShangwe kwa Vijana maarufu kwa Jina Serengeti Boys baada ya kuibuka Kidedea kwa bao 2-0 kwa kuitandika Burundi (U17) kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba leo.