Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali imeahidi kuwa italirejeshea Shirika la Posta Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 3.2 ambazo ilizitumia kuwalipa wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki ifikapo kufikia 30 Juni mwaka huu itakuwa imelipa kiasi cha Sh. Bil.3.2 zinazodaiwa na Shirika la Posta Tanzania

Ahadi hiyo imetole Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na MIpango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ludewa, Mhe. Deo Ngalawa (CCM), aliyehoji Serikali ilikuwa na mpango gani wa kuwalipa Wastaafu hao yenyewe moja kwa moja bila ya kutumia fedha za mfuko wa Shirika hilo.

‘’Shirika linasuasua kujiendesha, fedha ambazo zilikuwa zitumike kwenye operation ndizo hizo zimekuwa zikitumika kuwalipa Wastaafu wa Afrika Mashariki ili kulinusuru Shirika hilo serikali haioni umuhimu wa kulipa deni hilo”.alihoji Mhe. Ngalawa.

Mhe, Ngalawa alitaka kujua kwanini Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mwaka 2016 ilifungia akaunti za Shirika la Posta Nchini, kutokana na kuliidai Shirika hilo kiasi cha Sh. Mil.600, ikiwa Shirika hilo linaidai Serikali kiasi cha Sh. Bil.5.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha fedha hizo zinalipwa na Serikali yenyewe na sio Shirika.
Naibu Waziri wa Fedha na MIpango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...