Naibu Waziri wa Kilimo Uvuvi na Ufugaji Mhe. William Ole Nasha akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.

Na Daudi Manongi-MAELEZO DODOMA.
Serikali imesema kuwa inaandaa utaratibu wa kuunda Bodi mpya ya wakurugenzi ya Tumbaku  kwa kuwa ina umuhimu mkubwa katika ukuaji wa Sekta ya Tumbaku nchini.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge mjini Dodoma.

“Serikali ilivunja Bodi ya Tumbaku kwa lengo la kufanya maboresho katika utendaji kazi wa Bodi,na hatua hii ya kuvunja Bodi ya wakurugenzi haihusu kusitisha shughuli zinazotekelezwa katika sekta hii ya tumbaku kwani wapo wataalamu wanaoendeleza utekelezaji wa mpango uliopo wa kuendeleza zao la tumbaku”. Aliongeza Mhe.Ole Nasha.

Aidha amesisitiza kuwa upatikanaji wa pembejeo za zao hilo zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika kwa kila eneo kwa kupitia mchakato wa zabuni unaosimamiwa na kuratibiwa na vyama vikuu vya ushirika.

Amezitaja pembejeo za muhimu kwenye zao la tumbaku kuwa ni mbolea aina ya NPK, Mbolea aina ya CAN, nyuzi za kufungia tumbaku wakati wa kuvuna na wakati wa masoko zote zitapatikana kupitia vyama vikuu vya ushirika.

Ameeleza kuwa kwa kuzingatia kuwa wakulima wanahitaji huduma muhimu  hasa katika kipindi hiki cha kuelekea masoko ya tumbaku kwa msimu wa 2017/18, Serikali imeateua timu kwa ajili ya uratibu na kusimamia masuala hayo.

“Tuna timu tayari iko mkoani Tabora ambayo itasimamia na kuratibu masuala mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuandaa upatikanaji wa pembejeo kwa msimu ujao,hivyo pamoja na WETCU kuvunjwa kazi za chama hicho zinaendelea kama kawaida”Alisema Mhe.Ole Nasha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...