Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Antony Mavunde(katikati)akikata utepe kuashiria Uzinduzi rasmi wa duka jipya la VodacomTanzania Plc lililopo eneo la Kizota mjini Dodoma ,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo ,Jacqueline Maturu na kushoto ni Mkuu wa maduka ya rejareja na mauzo wa kampuni hiyo, Brigita Stephen.

Naibu Waziri wa Kazi Vijana na Ajira,Mh.Antony Mavunde, ameipongeza kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc kwa kuzidi kuimarisha huduma zake mkoani Dodoma hususani kipindi hiki ambacho Serikali imehamishia makao yake mkoani humo na ofisi nyingi za serikali zikiwa zinazidi kuhamia.

Akizindua duka jipya na la kisasa  la kampuni hiyo eneo la Kizota mwishoni mwa wiki,Mh.Mavunde alisema kuwa serikali inatambua kuwa sekta ya mawasiliano inachochea maendeleo ya nchi haraka ndio maana imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta hii ili kuwezesha wawekezaji kusambaza huduma za mawasiliano nchini kote,maeneo ya mijini na vijijini.
Mkuu wa maduka ya rejareja na mauzo wa Vodacom Tanzania PLC ,Brigita Stephen na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo ,Jacqueline Maturu wakimshuhudia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Antony Mavunde(katikati)akikata keki kuashiria Uzinduzi rasmi wa duka jipya la kampuni hiyo mwishoni mwa wiki lililopo eneo la Kizota mjini Dodoma.

“Nawapongeza Vodacom kwa kuongeza nguvu ya huduma zenu kwa kufungua duka jipya mbali na maduka yaliyopo,hatua hii inadhihirisha kuwa mnaenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya kuhamia Dodoma ambapo tayari shughuli nyingi za serikali zinafanyika mjini hapa na idadi ya wakazi inaongezeka hivyo mawasiliano bora yanatakiwa.”Alisema

Aliwataka wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa  mbalimbali zinazojitokeza  kama vile kutembelea duka  hili jipya la Vodacom kwa aili ya kupata huduma za mawasilaino ikiwemo kujua  huduma za kubadilisha maisha ya wananchi zinazotolewa na kampuni ya Vodacom bila kusahau kujitokeza kununua hisa zake katika mchakato wa kuuza hisa unaoendelea.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Antony Mavunde katikati akigongesha glasi wenye mvinyo ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa duka jipya la kisasa eneo la kizota mjini Dodoma.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu,alisema Vodacom itaendelea kutekeleza dhamira yake ya kurahisisha  mawasiliano na kufanya ubunifu wa kiteknlojia kupitia mtandao wake  lengo kubwa likiwa ni kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidijitali.

 “Tutaendelea kushirikianana na serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakua zaidi na inaleta mabadiliko mengi kwenye maisha ya watanzania na nchi nzima kwa ujumla. Vodacom imejikita kwenye kupanua wigo wa mawasiliano kuhakikisha kila mtanzania popote alipo anaweza kuwasiliana kwa bei nafuu, kupitia mtandao bora na wenye huduma zenye uhakika”.Materu

Kampuni ya Vodacom ambayo ni ya kwanza kuanza mchakato wa kuuza hisa zake katika sekta ya mawasiliano nchini  imekuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya mawasiliano kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubunifu na manufaa makubwa kwa jamii, hivyo kuchangia kwa kiasi kukubwa sana kuendeleza sekta hii muhimu kupitia njia mbali mbali kama kutoa ajira, kuchangia pato la taifa, kuchangia maendeleo ya jamii na kuwezesha watanzania wajiendeleze kiuchumi na kijamii kupitia mawasiliano ya bei nafuu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Antony Mavunde(katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC baada ya kuzindua rasmi duka jipya la VodacomTanzania Plc lililopo eneo la Kizota mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...