WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa waajiri wote nchini kujisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) kama sheria inavyotaka.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi duniani yaliyofanyika Aprili 28,2017 kitaifa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro, alisema bado kuna mwamko mdogo kwa waajiri kujisajili katika Mfuko huo. 

“Serikali inathamini sana juhudi zenu kama waajiri katika kuajiri wafanyakazi, niwaombe sana Chama Cha Waajiri nchini tushirikiane katika kuongeza hamasa ya kujisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ili hatimaye, Wafanyakazi wenu waweze kupata stahiki (Mafao), zao pindi wapatwapo na matatizo ya kiafya wanapokuwa kazini,” alisema Waziri Mhagama. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary 

Alisema mwitikio mpaka sasa kati ya waajiri 23,000 waliowabaini 700 pekee ndiyo wamesajiliwa katika mfuko huo hivyo kuiomba serikali isaide kuhamasisha waajiri wajisajili kwenye mfuko huo. 

Katika hatua nyingine Dkt. Omary alisema katika kipindi cha Mwezi Julai,2016 mpaka Machi 31,2017 wamepokea taarifa ya matukio 478 kutoka kwenye maeneo ya kazi. 

Alisema kati matukio hayo 478,matukio ya ajali ni 454,magonjwa sita na vifo 18 katika maeneo ya viwandani,migodini na vyombo vya usafiri ambapo waliopata ajali huduma ya fao la matibabu 

Aidha alisema mfuko huo unatoa mafao 7 ambayo ni mafao ya huduma ya matibabu,malipo ya ulemavu wa muda,malipo ya ulemavu wa kudumu,malipo ya anayemhudumia mgonjwa,huduma za ukarabati na ushauri nasaha,huduma za mazishi na malipo ya wategemezi. Angalia picha za matukio yaliyojiri katika banda la WCF katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amewataka waajiri nchini kujitokeza kwa wingi kujisajili katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (Workers Compesation Fund – WCF) kwa ajili ya kuwawezesha waajiriwa kupata mafao pindi wanapoumia,kuugua au kufariki wakiwa kazini. 
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano WCF, Laura Kunenge akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama katika banda la WCF wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi mwaka 2017 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary akiwasilisha mada fupi kuhusu Mfuko huo ambapo alisema walengwa wa mafao yanayotolewa na WCF kuwa ni wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi ambao wataumia au kuugua kutokana na kazi walizoajiriwa nazo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...