THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SERIKALI YAZINDUA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA HOSPITALI NCHINI

Serikali ya awamu ya tano nchini imezindua rasmi usambazaji wa vifaa vya hospitali kwa halmashauri zote nchini  katika kutekeleza mkakati wa kuboresha huduma za afya nchini kwa kuhakikisha wananchoi wanapata huduma kwa kiwango stahiki.

Akizindua usambazaji huo  leo wilayani Kongwa, Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema serikali imetekeleza ahadi iliyotoa kwa wananchi ambapo serikali inawekeza katika afya ya wananchi  hivyo kuweza kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Akizungumza kwenye hadhara ya wanachi wa Wilaya ya Kongwa,Waziri Ummy alisema serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo ya upatikanaji wa dawa ambapo bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 251 mwaka 2016/17.

“Hatua hii imeleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa dawa,vifaa na vifaa tiba kwenye vituo vya Umma vya kutolea huduma za afya,hivyo wanaomba wananchi kuhakikisha mnafika kwnye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata matibabu sahihi”.

Aidha, Waziri Ummy alisema kufuatia ahadi ya Mhe. Rais ya kununua na kusambaza vitanda kwenye vituo vya Umma ,Wizara yake kwa bajeti ya mwaka 2016/17 ilitenga kiasi cha shilingi biliuoni 4 za kuwezesha kununua pamoja na kusambaza  vifaa hivyo kwa halmashauri 184 nchini.

Alivitaja vifaa vilivyonunuliwa na kuvikabidhi kwa Mhe. Job Ndungai (Mb), Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania  Mhe. John Ndugai  ni pamoja na  vitanda vya hospitali (20),vitanda vya kujifungulia wajawazito (5), magodoro (25) na mashuka (50).

Vifaa vya Hospitali vitakavyopasambazwa kwenye Halimashauri zote 184 nchini ni pamoja na vitanda vya hHospitalini 3,680; vitanda vya kujifungulia akinamama wajawazito 920; magodoro 4,600; na mashuka 9,200. Thamani ya vifaa hivi ni shilingi bilioni 2,933, 125,600. Zoezi la kugawa vifaa hivi linatarajiwa kukamilika kabla ya Juni 30, 2107.

Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Ndugai ameishukuru Serikali kwa msaada wa vifaa vilivyotolewa kwa Hospitali na vituo vya Afya katika mkoa wa Dodoma ikiwemo Halmashauri Kongwa. Vifaa hivyo vitaboresha afya ya wananchi wa jimbo la Kongwa na maeneo mengine nchini na hivyo kusaidia kuwawezesha wananchi kukutumia mudao wao mwingi katika shughuli za kiuchumi.