THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SHERIA ISEMAVYO KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA MMILIKI ARDHI, NA GHARAMA ZA KUKIUKA SHERIA ZA UMILIKI

Mwananchi yoyote ana haki ya kupatiwa Hatimiliki ambayo ni nyaraka halali ya umiliki wa ardhi baada ya kupata ridhaa ya Kamishna au Kamati na kulipa ada stahili. Hatimiliki hutolewa ndani ya siku 90 mpaka 180 baada ya ridhaa husika. 
Katika fungu la 32 la Sheria ya Ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999, masharti ya umiliki wa ardhi yanaainishwa kuwa ni ya aina tatu, ambayo ni; Umiliki wa miaka 33, umiliki wa miaka 66 na umiliki ulio mkubwa zaidi ni wa miaka 99. 
Aidha, katika fungu la 33 la Sheria ya Ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999, inaeleza sharti la mmiliki wa ardhi katika kutoa malipo ya pango la Ardhi kwa kila mwaka wa fedha unapoanza. 
Mwananchi hana budi kutimiza masharti ya ulipaji kodi ya pango la Ardhi kwa wakati. Mwananchi anapokiuka sharti hili; fungu la 49 – 50 la Sheria ya Ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999 inaeleza gharama zake ni pamoja na kutozwa tozo au riba, Kupelekwa Mahakamani na Kufutiwa umiliki wa ardhi. 
 Mwananchi zingatia ulipaji wa Kodi la Pango la Ardhi, kutimiza wajibu wako, kuondoa usumbufu na kuongeza pato la Taifa Letu. Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mwanasheria Rachel Kilasi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , akifafanua sheria ya Ardhi na. 4 ya mwaka 1999 sambamba na Umiliki wa Ardhi (Haki, Wajibu na uzingatiaji wa ulipaji wa Pango la Kodi ya Ardhi kwa Mmiliki).