Msongola, Dar es Salaam.

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka watendaji wa Manispaa kuhakikisha wanazuia shughuli za kibinadamu ikiwemo ujenzi na kilimo katika maeneo oevu ili kulinda mazingira.

Amewasisitizia wananchi umuhimu wa kupanda miti mingi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuzuia magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa yakisababishwa na hali ya hewa.Mjema amesema hayo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti duniani, ambayo wilaya ya Ilala iliyafanya shule ya msingi Yangeyange katika Kata ya Msongola wilayani humo.


Alisema mbali na kutunza mazingira na kuleta mvua, miti imekuwa ikitumika kama dawa na jambo la muhimu ni kuwa miti hiyo inafyonza mionzi inayotoka katika jua. “Miti hii inafyonza mionzi mikali inayotoka kwenye jua, ile mionzi badala ya kuja kutugonga moja kwa moja kwenye ngozi zetu inapita kwanza kwenye miti, miti hii inatukinga na maradhi hasa ya kansa. Lakini sasa mkiangalia maradhi ya kansa yanazidi hasa ya ngozi, miti tunakata sana, tupande na tutunze miti,” alisema mjema.

Akizungumzia kuhusu wananchi wanaojenga katika maeneo oevu na mabondeni, aliwataka watendaji na wenyeviti wa maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo kuhakikisha wanazuia mapema ujenzi huo badala ya kusubiri mtu anamaliza ujenzi na ndipo waende kumhoji.
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akipanda mti wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Upandaji Miti, kilichofanywa na Wilaya ya Ilala katika shule ya Msingi, Yangeyange, Kata ya Msongola wilayani humo mkoani Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo ya Ilala Edward Mpogolo na Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...