NA VICTOR MASANGU, KIBAHA.
KATIKA kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano kupambana na wimbi la umasikini taasisi ya Namelok ya Wilayani Kibaha inatarajia kujenga kituo maalumu cha wasichana  na wanawake wajasiriamali ambacho kitakuwa kinajihusisha na masuala ya  utoaji wa mafunzo  mbali mbali kwa lengo la kuweza  kuwapa fursa ya  kuachana na kuwa tegemezi na kujiajiri wao wenyewe.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho zilizofanyika katika Kata ya Mwendapole  iliyopo  katika halmashauri ya mji wa Kibaha  Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Janet Mwasuka amesema kukamilika kwa ujenzi  huo kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa kuwainua wanawake  hao kiuchumuni  kupitia  mafunzo ya stadi za kazi pamoja na  fursa zilizopo  kutokana na elimu watakayoipata.

Janet alibainisha kuwa anatambau kuwa wanawake wegine katika Wilaya ya Kibaha ambao baadhi yao wameshindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa elimu ya ujasiriamali hivyo ana imani kituo hicho kitaweza  kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wanawake pamoja na jamii yote kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Purple Planet ya Jijini Dar es Salaam inayojishughulisha na  kuwasaidia katika kuendesha biashara zao na kuwainua kiuchumi wanawake wajasiriamali  Hilda Kisoka  amebainisha kuwa mikakati yao waliyojiwekea ni kufika mbali zaidi na kuuza bidhaa  wanazozizalisha hapa nchini  hadi nje ya nchi kwa lengo la kujitangaza zaidi.

Alisema kwamba ana imani wanawake wengi hapa nchini wana uwezo mkubwa wa kuengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu hivyo ameiomba serikali ya awamu ya tano kuwasaidi kwa hali na mali ili kuweza kufika mbali katika kuleta ushindani zaidi  wa masoko katika nchi zingine za nje na kuondokana na kuwa tegemezi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia  Happiness Seneda akionyeshwa eneo lililopo kata ya Mwendapole na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Namelok Janet Mwasuka wa  kushoto ambapo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili ya wasicahna na wanawake wajasiriamali  waliopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani (PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia Happiness Seneda kulia akiwa amemshika mmoja wa watoto huku akisikiliza maelekezo kuhusina na ujezni wa kiutuo hicho maalumu cha elimu kwa ajili ya wasichan na wakinamama kinachijengwa katika kata ya Mwendapole Wilayani Kibaha, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Namelok Janet Mwasuka.
  Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Nameloc akoinyesha eneo ambalo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili ya wasichana na wanawake wajasiriamali katika kata ya Mwendapole  Wilayani Kibaha Mkoani Pwani

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...