SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limetoa viwango bora vya soka duniani kwa nchi zote huku Brazil wakiwashika namba moja wakifuatiwa na Argentina na Ujerumani iliyoshika nafasi ya tatu.

Katika viwango hivyo bora vya soka, timu ya Misri iliweza kuingia katika 20 bora kwa kushika nafasi ya 19 na Senegal kushika nafasi ya 30 duniani.

Kulingana na ratiba ya mechi za Kirafiki za kalenda ya FIFA, Tanzania imefanikiwa kupanda kwa nafasi 22 kutoka 157 mpaka nafasi ya 135 .


Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki, Uganda imeendelea kuongoza lakini wakipanda  kwa nafasi 2 kutoka 74 mpaka 72 akifuatiwa na Kenya iliyo nafasi ya 78, Rwanda nafasi ya 117 na Burundi 141.

Viwango vingine vitatolewa Mei mwaka huu.


MATAIFA YA AFRIKA 10 YENYE VIWANGO BORA VYA FIFA AFRIKA MWEZI HUU . 

1. Misri ( 19 )

2. Senegal ( 30 )

3. Cameroon ( 33 )

4. Burkinafaso ( 35 )

5. Nigeria ( 40 )

6. Congo DR ( 41 )

7. Tunisia ( 42 )

8. Ghana (45 )

9. Ivory Coast ( 48 )

10. Morocco ( 53 )

MATAIFA 10  YENYE VIWANGO BORA VYA FIFA MWEZI HUU

1Brazili 

2.Argentina 

3.Ujerumani

4.Chile

5.Colombia

6.Ufaransa

7.Ubelgiji

8.Ureno

9.Uswisi

10.Hispania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...