Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu) kilichotokea tarehe         13 Aprili 2017.
Marehemu Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu)  alizaliwa tarehe 13 Novemba 1944, mtaa wa Uhuru,  Tarafa ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.  Alisoma na kuhitimu Shule ya Msingi mkoani Dar es Salaam na baadaye kuendelea na masomo ya Sekondari katika Shule ya Sekondari St. Joseph Convert School, Dar es Salaam hadi alipohitimu Kidato cha Nne mwaka, 1963.

Marehemu Brigedia Jenerali Albert Costantino Frisch (mstaafu), alijiunga na JWTZ tarehe 07 Desemba 1964 na kutunukiwa Kamisheni tarehe 22 Juni 1967.  Alistaafu Utumishi Jeshini kwa Heshima tarehe 30 Juni 1999.
Katika utumishi wake Marehemu alishika Nyadhifa mbalimbali Ikiwemo Mkaguzi Mkuu wa Jeshi Makao Makuu mpaka anastaafu.
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 20 Aprili 2017 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kuanzia saa 10:30 Asubuhi.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI ALBERT COSTANTINO FRISCH (MSTAAFU)
AMINA

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...