Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari (kushoto) akisaini mkataba na Naibu Mkurugenzi wa Kampeni  ya China Industrial Forum, Wang Xiangncheng ikiwa ni Makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya uwekezaji. Makubaliano hayo yamefikiwa kifuatia ziara iliyoratibiwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Balozi Mbelwa Kairuki pamoja na Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Tanzania kupitia TIC.Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na TPSF na kudhaminiwa na Exim Bank, Kaimu Mkurugenzi wa TIC alielezea kuwa mkataba huo ni muendelezo wa ushirikiano wa nchi hizi mbili ulioanza zamani na kusisitiza uendelee ili kuleta tija kwa nchi zote mbili. Ametoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta za Viwanda, Kilimo, umeme na mafunzo ya ufundi stadi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...