Frank
Mvungi-Maelezo.
Serikali
imezindua mfumo wa Kielektroniki wa Uhakiki wa Vibali vya ukazi “e-verification” hapa
nchini ili kuongeza tija na kudhibiti upotevu wa mapato. Kauli hiyo
imetolewa Jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna
Makakala wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo huo.
Akizungumzia
mfumo huo Kamishna Jenerali Makakala amesema utasaidia Makampuni, Taasisi, Mashirika na watu binafsi kuhakiki vibali vya
watumishi wao ili kuona kama ni halali ama
si halali na idara hiyo itakuwa tayari kuwasaidia wale wote watakaokuwa
na matatizo kupata ufumbuzi wa changamoto zao.
“Idara
inatoa siku 90 kwa watu wote kuhakiki vibali vyao vya ukazi ili kama wana
matatizo wasaidiwe kupata ufumbuzi” Alisisitiza Dkt Makakala.
Akizungumzia
lengo la mfumo huo Makalala amesema utasaidia kuimarisha udhibiti wa wageni
wanaoishi hapa nchini na kuzuia mianya ya upotevu wa maduhuli ya Serikali na
mfumo huo ni rahisi na unatoa fursa kwa wageni wote wenye vibali vya ukaazi
kuhakikiki kumbukumbu za vibali vyao ili kujua kama vimetolewa na Idara hiyo.
Aidha,Idara
ya Uhamiaji inawaomba wadau wa huduma zake kufika wao wenyewe katika Ofisi zao
katika ngazi ya Wilaya, Mikoa na Makao
Makuu kwani huduma za Uhamiaji hazina uwakala.
Mfumo huo wa
uhakiki wa vibali vya ukaazi kwa kutumia njia ya kielektroniki “e-verification”
unapatikana kupitia tovuti ya uhamiaji ya www.immigration.go.tz
Kamishna
Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo
mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama “E –
Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akizungumza
na maafisa Uhamiaji na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mfumo
mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama “E –
Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maafisa Uhamiaji na waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Afisa
TEHAMA, Mkaguzi wa Uhamiaji Sokolo Kaseko akifafanua na kuelekeza mbele
ya Waandishi wa Habari jinsi ya kufanya Uhakiki wa Vibali Ki-
elektroniki wakati wakati wa Uzinduzi wa Mfumo Uhakiki wa Vibali vya
Ukaazi ki-elektroniki uliofanyika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya
Uhamiaji, Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa
Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akifuatilia jambo wakati
wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi
ujulikanao kama “E
– Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Afisa
Utawala na Fedha wa Uhamiaji Edward Chegero na kushoto ni Afisa wa
vibali na Pasi wa Uhamiaji Musanga Etimba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...