Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii 

VIJANA wanaoandaliwa na chuo cha kodi nchini wanatakiwa kuangaliwa kwa jicho pana zaidi kwani hao  ni hazina kwa taifa katika masuala ya kodi na ushuru wa Forodha. 

Hayo ameyasema leo , Meneja wa Mafunzo na Maendeleo ya Watumishi wa TRA, Yassini Mwita wakati siku ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam, amesema kuwa wanafunzi wameonyesha umahiri katika masuala ya kodi ambapo ni hazina ya taifa watapotoka katika chuo hicho.

Amesema wanafunzi wamewasilisha maada mbalimbali juu ya ukusanyaji wa kodi na forodha kwa kile ambacho walifundishwa darasani na kufanyia kazi kwa mazingira na sheria watakayokutana nayo pindi wanapohitimu katika chuo hicho .

Mwita amesema wanafunzi hao wakitoka wanaweza kusaidia makampuni juu ya ukokotoaji wa kodi kuliko kampuni ikawa inafanya yenyewe bila kuwa na mtaalamu wa masuala ya kodi.

Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi, Nadhiru Juma amesema siku ya wanafunzi wa chuo hicho ni muhimu kutokana na wanafunzi kuonyesha uwezo wa darasani na jinsi watavyofanyia kazi kile ambacho wanakisomea.

Amesema kuwa wanafunzi wameonekana kuiva kwa kile kinachofundishwa katika chuo hicho na kuweza kufanyia kazi kwa weledi taifa lao katika masuala ya kodi na ushuru wa forodha.
Meneja wa Mafunzo na Maendeleo ya Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Yassini Mwita akizungumza na waandishi habari juu siku ya wanafunzi wa chuo cha kodi wakizungumzia namna ya kuwaandaa wanafunzi hao kuja kuhakikushha wanazisaidia makampuni katika Ukokotoaji wa Kodi leo jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Kutoa Alama kwa Wanafunzi wa Chuo Kodi Tanzania , Pili Marwa akizungumza katika siku ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi na kuwataka kujiandaa kuja kuisaidia serikali katika ukusanyaji wa kodi na ushuru wa Forodha leo jijini Dar es  Salaam.
Mwanafunzi wa Chuo cha Kodi , Charloite Adamu akionyesha umahiri wakati wa kuwasilisha mada katika siku ya wanafunzi wa chuo hicho uliondeshwa na Mamlaka na Mapato Tanzania (TRA) leo  jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wanafunzi wa Chuo cha Kodi wakifatilia maada katika siku ya kodi ya chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.


Afisa Uhusiano wa TRA, Oliver Njunwa akizungumza wakati ushereheshaji wa Siku ya Wanafunzi wa Chuo cha Kodi leo jijini Dar es  Saalaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...