THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WANAHABARI 66 KUWANIA TUZO YA UMAHIRI KATIKA UANDISHI WA HABARI 2016

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Waandishi wa Habari  66 kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari Jumamosi ya Aprili 29, 2017 wanatarajia kuchuana vikali katika shindano la kuwania Tuzo ya Umahiri katika tasnia hiyo.

Waandishi hao ni kutoka vituo vya Redio, Runinga (Television) na Magazeti ambao hapo awali walikua 810, ambapo pia walichujwa na kufikia 66. Kati yao wateule 36 kutoka kwenye Magazeti, 16 Redio na 14 Runinga, wakati kati yao 20 ni Wanawake, 9 wanatoka kwenye Magazeti, 14 kwenye Runinga (TV).
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandali ya Tuzo hizo (EJAT), Kajubi Mukajanga amesema kuwa kwa muda wa wiki moja katikati ya Mwezi kati ya tarehe 6 – 13 Aprili, 2017, Majaji  nane wamekuwa wakipitia kazi za Waandishi hao na baadaye kutambua zenye ubora.
Amesema kuwa idadi imeshuka kulingana na Mwaka uliopita kutokana na Mwaka uliopita idadi yao walikua Waandishi 84 waliofuzu kwa ubora wa kazi zao.
Kajubi amesema kuwa maoni ya Majaji kulikua na hamasa kubwa ya kuleta kazi lakini amesema kuwa nyingi hazikufikia vigezo, na hivyo kupelekea ugumu kuchagua wateule. 
Katika zoezi hilo jopo la Majaji liliongozwa na Jaji Valerie Msoka, Ndimara Tegambwage, Hassan Mhelela, Pili Mtambalike, Mwanzo Millinga, Nathan Mpangala na Dkt. Joyce ambaye alikuwa Katibu wa Jopo.

Shughuli ya ugawaji Tuzo hiyo utafanyika jijini Dar es Salaam, siku ya Jumamosi, Aprili 29 katika Hoteli ya Bluepearl na kuhudhuriwa na Mgeni rasmi ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya Mafanikio katika Maisha ya Uandishi wa Habari, 2015, Jenerali Ulimwengu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri katika Uandishi wa Habari (EJAT), Kajubi Mukajanga akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utoaji wa Tuzo hizo za Umahiri kwa Waandishi 66 kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari.