THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

wafanyakazi 16 wa Kampuni ya Quality Group wahukumiwa kwenda jea miaka mitatu au kulipa faini.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wafanyakazi16 wa Kampuni ya Quality Group, kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya jumla ya sh. Milioni 22.

 Washtakiwa hao wametiwa hatiani baada ya wiki iliyopita kukiri mashtaka yao mahakamani hapo.Katika Hukumu hiyo, washtakiwa kila mmoja amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu katika kila kosa au kulipa faini ya sh. Milioni 1.5 kila mmoja katika kila kosa katika makosa matatu.

Washtakiwa hao walikuwa wanatuhumiwa  kwa mashtaka matano likiwemo la kufanya kazi nchini kinyume na sheria na kuzuia maofisa Uhamiaji kutimiza majukumu yao.

Washitakiwa wote wametiwa hatiani leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.Hata hivyo, washitakiwa hao waliachiwa huru baada ya kulipa faini hiyo na kukwepa kifungo hicho.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Jose Kiran (40), Prakash Bhatt (35) ambao kwa pamoja walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya kuzuia maofisa wa Uhamiaji kufanya kazi yao.

Wengine ni  Rajat Sarkar (35), Jagadish Mamidu (29), Niladri Maiti (41) Divakar Raja (37) ambao ni washauri wa kampuni hiyo, huku Mohammad Shaikh (44) mhasibu na Pintu Kumar (28) ambaye ni Meneja msaidizi wa kampuni.

Wengine ni,  Bijenda Kumar (43), Prasson Mallik (46), Nipun Bhatt (32), Anuj Agarwal (46), Varun Boloor, Arun Kateel (46), Avinash Chandratiwari (33) na Vikram Sankhala (50) wote walikuwa wanakabiliwa na mashitaka matatu ya kukutwa na visa za kughusho na kufanya kazi nchini kinyume cha sheria

Hakimu Mkeha amesema,  washitakiwa 14 kila mmoja atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 1.5 kwa makosa matatu huku washitakiwa wawili wote kwa pamoja faini ya Sh milioni moja kwa kosa moja.

Imedaiwa kuwa, Februari 20, mwaka huu washitakiwa Jose Kiran, na Prakash Bhatt waliwazuia maofisa uhamiaji kutimiza majukumu yao baada ya kukataa kuripoti kwa Ofisa Uhamiajiwa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kujaribu kukimbia nje ya nchi kupitia mpaka wa Horohoro.

Ilidaiwa kuwa kwa washitakiwa 14 wanadaiwa kutenda kosa hilo Februari 13 mwaka huu maeneo ya Kampuni ya Quality Group wilayani Ilala mkoa wa Dar es Salaam.

Imedaiwa kuwa washitakiwa wote wakiwa ni raia wa nchini India, walikutwa na visa zilizoghushiwa kinyume na kifungu namba 31 (1) (e) na kifungu namba 2 cha sheria  ya uhamiaji ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho na sheria namba 8 ya mwaka 2015.

 Iliendelea kudaiwa kuwaalidai katika mashitaka ya pili kuwa washtakiwa hao walikutwa wakiishi nchini kinyume na sheria.Aidha katika shtaka la tatu, washtakiwa hao walikutwa wakifanya kazi nchini kinyume cha sheria.