Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, amewataka wananchi Mkoani humo, kutoa ushirikiano kwa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA, ili kuwabaini watu ambao si raiya wa Tanzania na wanalengo la kujipatia vitambulisho vya uraiya kinyume cha sheria za nchi.

Taarifa ya kitengo cha habari na Mawasilino cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imetanabaisha kuwa, Mkuu wa Mkoa ametoa rai hiyo katika viwanja vya Mashujaa mjini Mafinga, wakati akizindua zoezi la uandikishaji vitabulisho vya uraiya kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa, zoezi ambalo linaratibiwa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA.

Bi. Masenza, amesema, kabla ya ugawaji vitambulisho hivyo, NIDA wataendesha zoezi la kubaini watu ambao si raiya na wanania ovu ya kujipatia vitambulisho, hivyo akawataka wakazi wa Mkoa wa Iringa kuonesha uzalendo kwa kuwafichuo wale wote wasio na sifa za uraiya kwa usalama wa Taifa na watu wake.

Naye kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa vitambulisho vya Taifa NIDA Bw. Andrew Masawe, amesema mpaka sasa jumla ya Watanzania milioni 08 laki 04 na 99 elfu wametambuliwa na kukabidhiwa vitambulisho vya uraiya na kuongeza kuwa baada ya kukamilika kwa vitambulisho vya watumishi wa umma, zoezi hilo linaamia rasmi kwa wananchi na akawataka wananchi kuona umuhimu wa kutambuliwa kupitia vitambulisho hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akimkabidhi kitambulisho chake mmoja kati ya wakazi wa mji wa Mafinga wakati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza akihutubia wananchi katika viwanja vya Mashujaa mjini Mafinga.
Umati wa wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo kwenye kiwanja cha Mashujaa Mjini Mafinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...