Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI kwa kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw.   Wambura Sabora (hayupo pichani) wakati Mkurugenzi Mkuu huyo wa NBS alipofanya ziara mkoani humo hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo linavyoendelea.

Na Veronica Kazimoto
Imeelezwa kuwa asilimia 97 ya watanzania wanaoishi katika kaya zilizochaguliwa kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI katika mikoa 11 ambayo imeshafikiwa hadi sasa,  wameshiriki kikamilifu katika utafiti huo unaoendelea kufanyika nchini.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa utafiti huo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Wambura Sabora alipofanya ziara mkoani humo kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo linavyoendelea.
"Ninayo furaha kukutaarifu kwamba,  mpaka sasa utafiti huu umeshafanyika katika mikoa 11 ya Tanzania Bara pamoja  na visiwa vyote vya Zanzibar yaani Pemba na Unguja.  Jambo la kufurahisha zaidi ni mwitikio wa wananchi ambao ni asilimia 97 ya wanaoishi katika kaya zilizochaguliwa kwa ajili ya utafiti kukubali kushiriki," amesema Dkt. Chuwa.

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (kulia) akiwa na kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Wambura Sabora wakati Mkurugenzi Mkuu huyo wa NBS alipofanya ziara mkoani humo hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI linavyoendelea.
Mikoa ambayo imekamilisha utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI ni pamoja na Singida, Dodoma, Manyara, Iringa, Njombe na Ruvuma. Mikoa mingine ni Mbeya, Songwe, Katavi, Tabora na Kigoma.
Nae Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Wambura Sabora amemwambia Mkurugenzi Mkuu wa NBS kwamba, zoezi la utafiti huo mkoani humo linaendelea vizuri na mpaka sasa hakuna tatizo lolote  lililoripotiwa ofisisini kwake.

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (katikati) akiwa na Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kukinga na Kuzuia Magonjwa (CDC) Dkt. Eunice Mmari (kulia) wakipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa wadadisi wanaofanya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Bw. Johnmark Obura wakati wa ziara iliyofanyika mkoani Kagera hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo linavyoendelea.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...