Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Izeduwa Derex-Briggs alipofika Wizarani tarehe 06 Aprili, 2017. Katika mazungumzo yao, Bi. Derex-Briggs alimweleza Mhe. Waziri maendeleo ya utendaji wa Kitengo hicho kwa Kanda na umuhimu wa uwepo wao hapa nchini. Pia alimtambulisha Bi. Hodan Addou, Afisa Msimamizi mpya wa Kitengo hicho hapa nchini. 
Mhe. Mahiga akiendelea na mazungumzo na Bi. Derex-Briggs huku Bi. Hodan Addou (kushoto), Afisa Msimamizi mpya wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa hapa nchini na Bi. Sekela Mwambegele (kulia), Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia. 
Bi. Derex-Briggs nae akimweleza jambo Mhe. Waziri 
Hapa Bi. Derex-Briggs (katikati) akimtambulisha rasmi Bi. Addou kwa Mhe. Mahiga 
Picha ya pamoja 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...