Waziri Mkuu
Mhe.Kassim Majaliwa atafungua maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi
kiuchumi yatakayofanyika mkoani Dodoma katika viwanja vya mashujaa
kuanzia tarehe 18-22 April 2017.
Akizungumza na waandishi wa
Habari Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi(NEEC) Bi.Beng’i Issa amesema Maonyesho hayo yameandaliwa na
Baraza hilo kwa lengo la kutoa elimu kwa umma juu ya huduma mbalimbali
zitolewazo na mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
“Tumeamua
kufanya maonesho haya kwa mara ya kwanza kwa sababu changamoto kubwa
tuliyonayo ni kuwa mifuko hii haifahamiki sana na wananchi, wengi
walikuwa hawajui wafanye nini ili waweze kupata fursa ya kupata mitaji
na kusaidiwa na mifuko hii ambayo imeanzishwa na Serikali kwa ajili
yao”,Aliongeza Bi.Beng’i.
Amesema maonyesho hayo yatawapa
wananchi fursa ya kuonana na watu ambao wamefanikiwa katika kipindi
kilichopita na hasa kujua jinsi gani watafaidika na mikopo ambayo
inapatikana kupitia mifuko hii.
Ameitaja mifuko ambayo
itashiriki ni pamoja na Mfuko wa kuendeleza wajasiriamali wananchi,
Mfuko wa Uwezeshaji wa Mwananchi, Mfuko wa Pembejeo za Kilimo , Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana, Mfuko wa Dhamana za mikopo kwa wajasiriamali
wadogo na wa kati na Mfuko wa Dhamana za Mikopo kwa Mauzo ya Nje ya
Nchi.
Mifuko mingine ni Mfuko wa kuwasaidia makandarasi,Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii,Mfuko wa Misitu Tanzania,SELF Microfinance Fund na
PASS Trust Fund.
Kauli mbiu ya Maonyesho haya ni “WEZESHA WANANCHI KIUCHUMI ILI KUJENGA UCHUMI WA KATI NA TANZANIA YA VIWANDA”
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi yatakayofanyika katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 18-22 April 2017.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akimsikiliza Mhasibu Mkuu kutoka Mfuko wa Rais wa kujitegemea Bw.Ahazi Kibona juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akizungumz ana waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi yatakayofanyika katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 18-22 April 2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...