Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani wa taifa la Israel,Ehud Barak walipokutana katika eneo la Olduvai Gorge katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro akiwa njiani kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (katikati) ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Pascal Shelutete.
Waziri Mkuu wa zamani wa Taifa la Israel,Ehud Barak (kushoto) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani baada ya kukutana katika eneo la Makumbusho ya kale la Olduvai Gorge ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro akiwa njiani kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (kushoto) ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.
Mhandisi Ramo Makani akimueleza jambo Waziri Mkuu wa zamani wa Taifa la Israel ,Ehud Barak baada ya kukutana katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro akiwa njiani kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani (katikati) akimongoza Waziri Mkuu wa zamani wa Taifa la Israel ,Ehud Barak (kushoto) kutembelea eneo la Olduvai Gorge .kulia ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete.
Waziri Mkuu wa zamani wa taifa la Israel ,Ehud Barak akitia saini katika kitabu cha wageni huku Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akishuhudia mara baada ya kufika eneo la Olduvai Gorge akiwa njiani kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushudia tendo la wanyama aina ya Nyumbu wahamao kwa makundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...