Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewataka wadau wa Utalii nchini kutoa maoni na michango yenye tija itakayopelekea upatikanaji wa Sera bora itakayoleta ufanisi katika uendeshaji wa huduma zinazotolewa katika sekta ya Utalii.

Hatua hiyo inakuja ikiwa, Sera ya Taifa ya Utalii iliyopo ilifanyiwa mapitio kwa mara ya mwisho mwaka 1999 ambapo ni takribani miaka 17 iliyopita.

Katika kutambua hilo, Wizara imeanza kupitia upya Sera hiyo ili kuhakikisha Sekta ya Utalii inakwenda sambamba na mabadiliko mbalimbali yanayotokea duniani yakiwamo ya teknolojia, kijamii, kiuchumi, kisiasa na mazingira

Akizungumza katika mkutano unaofanyika kwa muda wa siku mbili Jijini Arusha kwa mikoa ya kanda ya Kaskazini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki alisema Sera inafanyiwa marekebisho kwa kuwa imepitwa na wakati kutokana na mabadiliko makubwa yaliyotokea katika sekta hiyo.

Aidha, alisema kwa kutambua mchango wa utalii kiuchumi , ni wazi kuwa sera wezeshi ya utalii yenye kutoa mwongozo wa utaratibu bora na sahihi wa usimamizi, uendelezaji na utendaji katika sekta hiyo unahitajika.

’’ Tunataka kuibadilisha sera hiyo ili iweze kujibu changamoto za aina ya utalii wa sasa ambao kipindi cha nyuma haukuwepo, akitolea mfano utalii mikutano pamoja na utalii wa kiutamaduni ambao umekuwa ukikua kwa kasi hapa nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. KATIKA WIZARA AMBAZO ZINATAKIWA MABADILIKO YA HARAKA NI HII YA MALIASILI NA UTALII,MIMI NI MMOJA KATI WATU WENYE KILIO CHA KUINGIZWA KWENYE UMASIKINI HATA HAKI ZA BINADAMU HAZIPO KABISA NA MAAMUZI MABAYA AMBAYO YAMEFANYWA NA WIZARA HII YA MALIASILI NA UTALII,AMBAYO YAMEFANYWA NA WAZIRI WAKE BWA.PROFESSOR MAGEMBE.TULIFUNGIWA GHAFLA BIASHARA YA VIUMBE HAI HUKU WAFANYABIASHARA WAKIWA NA LESENI, WAMELIPIA VIBALI VYOTE,WANA VIUMBE HAI MAZIZINI,WENGINE WAKIWA WAMELIPIA BENKI KWA AJIRI YA VIBALI VYA KUKAMATA,WENGINE WAKIWA WAMESHAFANYA TARATIBU ZOTE ZA KULIPIA VETERNARY NA USAFIRI WA AIRLINES,WENGINE WAKIWA WAMESHAKAMATA WADUDU,NDEGE,MIJUSI NK,LAKINI WAZIRI HUYU BILA KUANGALIA ATHARI WANAZOKWENDA KUPATA WATANZANIA HAWA ANASITISHA BIASHARA GHAFLA KWA SABABU AMBAZO HAZINA MSINGI NA SI ZA KWELI.LEO HII VIUMBE HAWA WANAKUFA TU WATU HAWAWEZI KUENDELEA KULISHA VIUMBE HAWA,KWA KUWA HAKUNA FEDHA ZA KUNUNULIA CHAKULA ,WAPO WALIOPOTEZA NYUMBA ZAO KUTOKANA NA MIKOPO WANAYODAIWA NA MABENKI,TAASISI ZA FEDHA NA SACCOS NK,WENGINE WAMESHITAKIWA KATIKA MAHAKAMA ZA NJE KUTOKANA NA ADVANCES.KWA KWELI NI HUZUNI HII SERIKALI ILICHOWAFANYIA WATANZANIA HAWA KARIBU 1,000,000 WANAOTEGEMEA BIASHARA HII SI CHA KIBINADAMU.NI HUZUNI LICHA YA JUHUDI KUZIONA NGAZI MBALIMBALI AKIWEMO WAZIRI MKUU NA RAIS LAKINI NI MASIKITIKO TU HAKUNA ANAYEONA HILI TATIZO KUWA NI KUBWA CHA KUSIKITISHA NA KUJIULIZA KWA NINI SERIKALI ILICHUKUA FEDHA ZAO NA KWA NINI SERIKALI HII HAIWAJALI WATANZANIA HAWA WANAOTESEKA KWA FEDHA ZAO SASA WANAKUWA WATU WA KUTANGATANGA KUTAFUTA HAKI ZAO KWENYE SERIKALI AMBAYO HATA HAIWAJALI HUKU WAFANYABIASHARA HAWA WAKIPOTEZA MALI ZAO NA HAKI ZAO.VIUMBE HAWA WAKIENDELEA KUFA NA KUTUNZA WAKATI HATA HAWAJUI HATIMA YAKE .HUKU SERIKALI HII IKIJISIFIA KUWA INATAKA KUWA YA VIWANDA SIFIKIRII KWA HALI NJIA HII ITAKUWA YA VIWANDA,KAMA WATANZANIA WANAONEWA KWA HAKI ZAO NA FEDHA ZAO HAWA SIWAPIGA DEAL,WANADHULUMIWA NA SERIKALI YAO KWA HAKI YAO INASIKITISHA SANA.HAYA NDIYO MAMBO YANAYOWAFANYA WATANZANIA HAWA KUICHUKIA SERIKALI YAO KWA MATENDO YA MTU MMOJA AMBAYE ANAAMUA BILA HATA KUFIKIRIA KUWA HAWA WATANZANIA WANA LESENI,WAMELIPIA VIBALI VYOTE,WANAVIUMBE HAI,KIASI INAONEKANA SASA WATU HAWA NI KUICHUKIA SERIKALI HII KAMA YA WANYANYASAJI KATIKA NCHI YAO,TUNAOMBA WABUNGE MLIONE HILI.

    ReplyDelete
  2. Hakuna haki kabisa hapa na maamuzi mabaya ya kukurupa ndiyo yanayosababisha watu kuichukia serikali yao.hawa wanaona serikali yao haiwajali tena na wanazungushwa kwa kudai haki zao.Mh Rais ingilia kati kupata ukweli usisikilize upande mmoja wakati wananchi hawa wanaumia kwa haki zao.Inaelekea kuna tatizo hapa

    ReplyDelete
  3. Ndugu Mhariri wa Michuzi Blog shukrani kwa kutoa fursa hii adimu kutathimini Wizara hii ya Mali Asili na Utalii. Ukweli kabisa Waziri mwenye dhamana ya Wizara hii ni dikteta, kwa nini nasema hivi, mwaka mmoja uliopita aliamua peke yake bila ya kushauriana na wataalam wake wala wafanyabiashara wa viumbe hai kuwa biashara hii itafungwa na Serikali, yeye aliamua kutangaza kuwa biashara ya viumbe hai inafungwa tu bila ya mjadala.

    Huyu Waziri hakuzingatia kuwa wafanya biashara hawa wana mazizi yaliyohifadhi viumbe hai ambavyo vilikuwa vinasubiria kusafirishwa kutokana na oda mbalimbali kutoka wafanya biashara wa nchi za nje,pili wafanya biashara hawa wana leseni halali za kusafirisha viumbe hai ambazo hutolewa na Wizara ya Mali Asili na Waziri husika analitambua hilo kwa kuwa lipo kisheria, tatu viumbe hawa hai wanahitaji kulishwa na kutunzwa kwa kupatiwa huduma za matibabu kwa gharama kubwa.

    Wafanya biashara tunategemea mitaji toka kwenye taasisi za kifedha, na wengi wetu tulikopa kwa kuweka dhamana mbalimbali tukiamini tupo katika biashara ambazo ni halali na kwa kuwa tulikuwa na oda mkononi kutoka kwa wateja wetu ambao nao walitoa malipo ya awali ambayo yalitumika kukamatia viumbe hai na kusafirishia kutoka porini hadi kwenye
    mazizi yetu.

    Ukiangalia taswira nzima Waziri huyu alipaswa kutoa nafasi kwa wafanya biashara wasafirishe viumbe walivyokuwa navyo mazizini kwa kuwa walikuwa na vibali halali vya kusafirishia, kwa nini jambo hili aliamua binafsi kutoka moyoni mwake bila ya kushirikisha hata wataalam wake na wafanya biashara. Namakumbusha kwamba kitendo hiki cha kufunga biashara hii kimewasababishia hasara kubwa sana wafanyabiashara wa viumbe hai, wamepoteza dhamana zao, familia zao zinaishi kwa dhiki kubwa pamoja na kufukuzwa shule kwa watoto wao.
    Lawama zote hizi zinamwangukia Waziri Maghembe kwa kutotumia busara zake.

    Hata kama alifanya kosa kufunga bila ya kufuata taratibu za kisheria, lakini sasa asione aibu kurudi na kusema na kuwaomba radhi hawa wafanyabiashara na kuruhusu wasafirishe viumbe walivyo navyo mazizini ili angalau kufidia hasara walizopata kutokana na tamko lake ambalo tunaamini lilikuwa batili.

    Kipindi cha Serikali ya awamu ya nne Waziri Maige akiwa Waziri wa Mali Asili alimdanganya Waziri Mkuu wakati huo akiwa Mh. Mizengo Pinda akafunga biashara bungeni kwa kisingizio kuwa wafanyabiashara wa viumbe hai walihusika na utoroshaji wa twiga kinyume cha sheria, baada ya uchunguzi ilibainika kuwa vibali vilitolewa na ofisi yake Rais alimuajibisha pamoja na maofisa wake waandamizi katoka nafasi yake ya Uwaziri

    Kwa kipindi hiki ufungaji wa biashara yetu unatokana na Waziri Maghembe ambaye alidai kulikuwa na utoroshaji wa tumbili 62, baada ya uchunguzi na kesi iliyoamuliwa mahakamani iligundulika kuwa hapakuwa na utoroshaji na vibali vyote vilikuwa na vilitolewa Wizara yake.

    Taswira hii inafanana na ilivyotokea wakati wa Waziri Maige kulitokea na mgongano wa kimaslahi kati ya wazawa na mgeni [AHMAD KAMRAN} Mpakstan ambaye aliuziwa twiga wanne {4} kwa bei ya wote usd 8,000 badala ya usd 300,000.

    Mgogoro unaoendelea hivi sasa ambao umesababisha biashara kufungwa inatokana na mgongano wa kimaslahi kati ya wazawa na mgeni {David Zhorzholadaze} Mrusi.

    Wazawa walipata zabuni ya kupeleka ngedere 8,000 ambazo zinaruhusiwa kwenye matumizi ya kusafirisha kutoka kwenye mgao wa Taifa{NATIONAL QUOTA} Baada ya huyo mgeni kukosa zabuni hiyo ya kusafirisha ngedere ambayo alikuwa ameipania sana, kwa utumia ukwasi wake na washirika wake ambao walikuwa na ushawishi mkubwa kwenye awamu iliyopita ya utawala, alidai kuwa Ikulu ilikuwa kama nyumbani kwake, kutokana mgogoro huo ndiyo ulipelekea biashara ya viumbe hai kufungwa.

    Kitendo cha kusitishwa biashara hii kimesababisha Taifa kupoteza dola za kimarekani zaidi ya 8,900,000. {tsh 20 bn}

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...