Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipongeze Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kuendesha warsha ya siku tatu kuhusu upasuaji wa matundu madogo (laparoscopic surgery) kwa madaktari kutoka hospitali mbalimbali nchini.

Warsha hiyo ilianza jumatano na imemalizika leo Ijumaa na kuwashirikisha madaktari kutoka hospitali ya za jijini Dar es Salaam zikiwamo Kairuki, Tumaini, Regency na Agha kan. Madaktari wengine ni kutoka hospitali za umma zikiwamo Hospitali ya Temeke, Amana pamoja na hospitali za mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Morogoo na Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akimkabidhi cheti cha ushiriki Dk. Paul Kisanga wa Hospitali ya Selian mkoani Arusha leo.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara hiyo Dk. Dorothy Gwajima kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara, Dk. Mpoki Ulisubisya wakati akifunga warsha hiyo.

Dk  Gwajima amewataka washiriki wa warsha hiyo kupeleka ujuzi waliojifunza kwa madaktari wengine ili kupunguza msongamano wa wagonjwa wanakwenda kutibiwa katika hospitali ya Muhimbili.

“Kwa niaba ya wizara napenda kuipongeza Muhimbili kwa kuandaa mafunzo haya, sisi wizara tunawaunga mkono na msifikiri tumewasahau la hapana kwani tunatambua uwezo wa madaktari. Heshima ya hospitali itabaki pale pale kwani Muhimbili kitovu cha uwanzishwaji wa HospitaOceac road, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Mifupa ya Moi,” amesema Dk Gwajima.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima akifunga warsha ya siku tatu iliyolenga kuwajengea uwezo madaktari nchini kuhusu upasuaji wa matundu madogo (laparoscopic Surgery).

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amewashukuru madaktari kutoka hospitali za binafsi na umma kwa kushiriki kwenye mafunzo hayo.

“Tumeanzisha mafunzo haya na napenda kuwahakikishia tutaendelea kuandaa warsha kwa kada nyingine ili kuwajengea uwezo madaktari wa hospitali za mikoa na wilaya nchini,”amesema Profesa Museru.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar ameishauri uongozi wa Muhimbili kuendelea kutoa mafunzo hayo na kuendesha ufapasuaji wa njia ya matundu madogo kwa wagonjwa waliopo mikoani kwani wengi wao hawana fursa ya kupatiwa huduma hiyo.
 
Daktari bingwa wa Magonjwa ya Kinamama na Uzazi, Profesa Rafique Parkar (kushoto) akimfanyia upasuaji mmoja wa kinamama mwenye matatizo ya uzazi leo. Kulia ni Dk. Vicenti Tarimo akishirikiana na Profesa Parkar.

Washiriki walikabidhiwa vyeti baada ya mafunzo hayo kufungwa.

Katika hatua nyingine, wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kutumia njia ya matundu madogo wanaendelea vizuri na baada ya afya zao kurejea katika hali ya kawaida wataruhusiwa kurejea nyumbani.

Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji hadi leo wamefikia wanane.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...