Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii



IKIWA katika hali ya kuyumba kiuchumi na kushindwa kuwalipa wachezaji wao mishahara kwa wakati, neema imeanza kuwaangukia baada ya kampuni ya SportsPesa ya Kenya kutaka kuwamwagia fedha iwapo mkataba wao utafanikiwa.


Yanga itakuwa ni ya tatu kwa timu za Afrika Mashariki kuingia mkataba wa fedha nyingi iwapo watakapofanikiwa kumalizana kumalizana na Kampuni ya SportsPesa ya Kenya.

Iwapo mkataba huo utafanikiwa, Yanga na kampuni hiyo ya SportsPesa watasaini mkataba wenye thamani ya bilion 4.5 ambapo utakuwa ni wa miaka mitano ambapo kwa mwaka utakuwa na thamani ya Sh milioni 900.

Uongozi wa Yanga leo unatarajiwa kutakutana na wawakilishi wa kampuni hiyo, ambapo wakikubaliana wataingia mkataba huo wa miaka mitano ambao kila mwaka utakuwa na nyongeza ya asilimia sita ya fedha.

Awali, SportsPesa walileta mapendekezo katika klabu ya Yanga kuhusiana na mkataba huo lakini ulikatiliwa kutokana na mkataba huo kutokukidhi vigezo nan kuwa na maslahi na wakawapelekea mapendekezo yao na namna gani wanataka mkataba huo uweje.

"\Leo wawakilishi wa SportPesa watakutana na uongozi wa Yanga ili kumalizana nao juu ya mkataba wanaotaka kuingia na hiyo ni kutokana na kufika makubaliano ya kimkataba," kiisema chanzo kutoka kamati ya utendaji ndani ya klabu hiyo.

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, ambaye alisema wapo kwenye hatua za mwisho za kuingia mkataba na SportsPesa.

"Napenda nizungumze kitu kilichokua tayari au kimekamilika hatua ya kuingia mkataba na SportsPesa bado, ila tutakutana nao kwa mazungumzo ya mwisho ambayo yatatoa jibu kama watatudhamini au la.

"Tunazungumza na SportsPesa kwa kuwa hawa wamekuja moja kwa moja kwetu tofauti na kampuni nyingine ambazo zinataka kutudhamini, lakini ipo kampuni tuliyoipa jukumu la kufanya mazungumzo nao nasi kutuletea taarifa ya kila kinachoendelea." alisema Mkwasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...