Beki wa Yanga, Deus Kaseke akijarimu kumdhibiti Mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakar "Sureboy", katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara, uliochezwa jioni ya leo kwenye dimba la Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 1-0.

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Vodacom Tanzanja Bara Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa.



Mpira huo ulioanza majira ya sa 10 alasairi ulichezeshwa na Mwamuzi Jonesia Rukyaa akisaidiwa na John Kanyenye na Soud Lila ulikuwa na ushindani mkubwa huku Azam wakionekana kutawala sehemu ya kiungo.

Azam katika dakika 45 za kipindi cha kwanza walishindwa kutumia nafasi walizozipata kutokana na kutokuwa makini kwa safu yao ya ushambuliaji.

Kipindi cha pili kimeanza kwa kila upande kutafuta goli la kuongoza na katika dakika ya 71 mshambuliaji wa kimataifa kutoka Zambia Obrey Chirwa anaiandikia Yanga goli la kuongoza akitumia uzembe wa mabeki wa Azam kuurudisha mpira kwa golikipa Aishi Manula.

Yanga wanaamka na kuanza kulishambulia lango la Azam lakini nao wanakuwa makini na kusaka goli la kusawazisha na mpaka dakika 90 mwamuzi Jonesia anapuliza filimbi ya mwisho Yanga wanatoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 1-0.

Baada ya matokeo hayo, Yanga wanafikisha alama 56 wakiwa mbele kwa alama moja dhidi ya mahasimu wao Simba wenye alama 55 ambao wanacheza na Kagera Sugar katika Uwanja  wa Kaitaba mkoani Kagera.

Kikosi cha Yanga kilichoanza leo.
Kikosi cha Azam FC kilichoanza leo.
Mshambuliaji wa Azam, Shaban Idd akiipokea pasi kwa kisigino mbele ya Mabeki wa Yanga, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara, uliochezwa jioni ya leo kwenye dimba la Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 1-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...