Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akiwaongoza wanafunzi na baadhi ya wakufunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kucheza nyimbo ya “Strength of a woman” ya Mwanamuziki Shaggy ambayo ina maudhui ya kuwainua wanawake wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo hicho mwishoni mwa juma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha masuala ya jinsia wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr. Eugenia Kafanabo akizungumza wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo hicho mwishoni mwa juma.

Mkufunzi Mkuu na Msambazaji wa huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Kulwa Mbena akizungumza wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) chini ya udhamini wa Kampuni ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika siku ya jumamosi katika ukumbi wa Nkurumah uliopo chuoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (Kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) na kupata udhamini kutoka kwa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Nkurumah kwa ajili ya kuadhimisha hafla hiyo. Katikati ni Mkufunzi Mkuu na Msambazaji wa huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Kulwa Mbena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...