Jumuiya ya Watanzania katika Jiji la Leicester inapenda kuwatangazia Watanzania 
na wale wote wenye nasaba na Tanzania waishio Leicester na vitongoji vyake kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk. Asha-Rose Migiro anatarajia kufanya ziara ya mjini Leicester Jumamosi ya tarehe 22 Aprili 2017. 
Katika ziara hiyo Mh. Balozi
Migiro atapata fursa ya kuongea na Watanzania wote na pia kutembelea shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na wajasiriamali wa Kitanzania waishio Leicester. Ziara hii pia utawawezesha watanzania kumpatia Mhe. Balozi mawazo,
maoni na ushauri kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi kwa wanadiaspora na Serikali yetu kwa ujumla.
Mkutano utafanyika kuanzia saa nane kamili mchana kwenye ukumbi ufuatao:
Peepul Centre,
Orchardson Avenue,
Leicester,
LE4 6DP
Tunaomba Watanzania wote mjitokeze kwa wingi kumkaribisha Balozi wetu na kushiriki katika mazungumzo yatakayosaidia kuharakisha maendeleo ya
wanadiaspora na nchi yetu. Kuja kwenu ndio kufanikisha ziara hii muhimu. Tafadhali mjulishe mwenzio.

Asanteni kwa ushirikiano wenu.
JUMUIYA YA WATANZANIA LEICESTER



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...