Mhe. Fatma Mohammed Rajab, Balozi  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar akiwa katika mazungumzo na Mhe. Sultan bin Saad Al Muraikhi, Waziri wa Nchi, Mambo ya Nje wa Qatar. Mazungumzo hayo yalifanyika baada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho. Wawili hao walizungumza masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar.
Balozi  wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Mohammed Rajab akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Sultan bin Saad Al Muraikhi, Waziri wa Nchi, Mambo ya Nje wa Qatar ofisini kwa Mhe. Waziri. Mhe. Fatma Rajab anakuwa Balozi Mkazi wa kwanza kuiwakilisha Tanzania katika Taifa la Qatar. Mhe. Balozi alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Doha alipokelewa na Idara ya Itifaki ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar. Aidha, wawakilishi wa Watanzania wanaoishi nchini humo walifika Uwanja wa Ndege kumlaki
Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab, akiwa na viongozi wa Watanzania wanaoishi nchini Qatar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...