THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Balozi Seif akutana na Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akikiongoza Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar akiwa Mwenyekiti  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad akitoa taarifa ya tathmini ya awali ya athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Kanda ya Zanzibar Nd. Mohamed  Khamis Ngwali akitoa tathmini ya hali ya Mvua zinazoendelea kunyesha katika ukanda wa Pwani katika Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi , Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Nd. Mustafa Aboud Jumbe akitoa ufafanuzi wa hatua zilizochukuliwa na Wizara yake za kurekebisha baadhi ya miundombinu iliyoharibiwa na Mvua za Masika zinazoendelea kunyesha. Picha na – OMPR – ZNZ.