Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inasubiri kuyapokea kwa ajili ya kuyafanyia kazi mapendekezo yatakayowasilishwa ya Rasimu ya Sera ya Habari Zanzibar katika kuona Sekta ya Habari Nchini inakuwa imara. 

Alisema Taasisi zinazohusika na jukumu la kusimamia masuala hayo ni vyema zikahakikisha kwamba zinaharakisha mapendekezo hayo ili ile dhana ya Uhuru wa kupata Habari bila ya kuogopa inapatikana. 

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Uongozi wa Baraza la Habari Tanzania { MCT } ulioongozwa na Katibu Mtendaji wake Bwana Kajubi Mukajanga aliokutana nao hapo Afisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar. 

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutoa kila aina ya msaada katika kuona Sekta hiyo muhimu kwa jamii inawajibika ipasavyo katika kuwapasha Habari Wananchi. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) uliofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kubadilishana nao mawazo. Kulia ya Balozi Seif ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga na Kushoto ya Balozi ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan .
Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif walipokutana nae kwa mazungumzo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga Kulia ya Balozi Seif akielezea mikakati ya Baraza la Habari Tanzania inavyofanya kazi Zanzibar katika kuhakikisha Maadili ya Habari yanazingatiwa na Wana Habari wote Nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...