Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wadau wa Habari kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani hapo katika Chuo cha Habari Kilimani Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga, kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Mitawi.
 Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar Omar akitoa ufafanuzi juu ya Umuhimu wa Wanahabri kuzingatia suala la Amani katika uandishi wao wa kila siku.
 Viongozi wa Meza Kuu kutoka kulia Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga, Mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi Mh. Ayoub, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Nd. Hassan Mitawi wakifuatilia hafla ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari hapo Kilimani.
 Kikundi cha Utamaduni cha Mkoa Mjini Magharibi kilitoa Burdani katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari hapo katika Ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Mjini Zanzibar.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...