Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuifunga Mbinga Community Bank Plc, kusitisha shughuli zake zote za kibenki na kufuta leseni yake ya biashara ya kibenki kuanzia tarehe 12 Mei, 2016.


Aidha Benki Kuu ya Tanzania imeiweka Mbinga Community Bank Plc chini ya ufilisi na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia tarehe 12 Mei, 2017, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Benki Kuu leo asubuhi imeeleza.

Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa Mbinga Community Bank Plc ina upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki an Taasisi za Fedha ya wmaka 2006 na kanuni zake.

“Upungufu huu wa mtaji na ukwasi unahatarisha usalama wa sekta ya fedha, na kwamba kuendelea kwake kutoa huduma za kibenki kunahatarisha usalama wa amana za wateja,” taarifa hiyo imeeleza.

Aidha, Benki Kuu ya Tanzania imeuhakikishia umma kuwa “itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.”

Benki Kuu ya Tanzania imechukua uamuzi wa kuifunga benki hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 56(1) (g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2) (i), 11(3) (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...