Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii inaeleza kuwa leo saa tatu asubuhi imetokea ajali katika eneo la Rhotia Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha, iliyohusisha Basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St Lucky ya jijini Arusha, inayodaiwa kuwa ilipoteza mwelekeo na kupindukia korongoni wakati wakiwa safarini kuelekea Karatu waliokuwa wakienda kufanya mitihani ya ujiranimwema na wanafunzi wenzao wa Shule ya Tumaini English Medium ya mjini Karatu.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha, Afande Charles Mkumbo, wanafunzi 32 , walimu 2 na dereva wa gari hilo wamepoteza maisha huku wanafunzi wengine 4 na mtu mzima mmoja wakiwa wamejeruhiwa.
Chanzo cha ajali hiyo mbaya kutokea mkoani humo bado haijajulikana na uchunguzi unaendelea. Globu ya Jamii inatoa rambirambi kwa wafiwa na kuwatakia majeruhi nafuu ya haraka.
Umati wananchi ukiwa katika nje ya chumba cha maiti cha hospitali ya Mount Meru jijini Arusha kutambua miili ya wanafunzi na wanafunzi waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
R.I.P
ReplyDelete