NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema kinaendekea na juhudi za kuishauri serikali iharakishe utaratibu wa kutoa misaada kwa wananchi walioathiriwa na maafa ya mvua ili waweze kupata huduma za msingi kama walivyo wananchi wengine waliosalimika na tatizo hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar, Dkt.Abdalla Juma Saadala ” Mabodi” katika mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maeneo mbali mbali nchini yaliyopata maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Dkt.Mabodi aliwambia wananchi hao kwamba serikali ya Mapinduzi ya zanzibar inayotokana na chama hicho ni sikivu na inathamini maisha na utu wa wananchi wote bila ya kujali itikadi za kisiasa, hivyo itaendelea kutoa mapendekezo kwa Idara ya Maafa nchini ifike kila pembe ya visiwa vya zanzibar kuhakikisha wananchi wote waliopata maafa wanaratibiwa na kupatiwa misaada.

Alieleza kwamba pamoja na taasisi hiyo kufanya kazi za kisiasa bado ina jukumu la kuwalinda na kuwasaidia wananchi wakati panapotokea majanga mbali mbali ya kitaifa ili waweze kubaki salama na kuendelea na shughuli za kimaendeo.

” Wananchi tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atuvushe salama katika hii neema ya mvua iliyochanganyika na mitihani, ili turudi katika maisha ya kawaida na kuondokana na hofu.
Ni msafara wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” kulia mtu wa nne aliyafaa sare za CCM fulana na kofia za kijani huko shehia ya Koani Wilaya ya Kati Unguja.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” akizungumza na mmoja kati ya wananchi waliopata maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha, Bw. Kassim Vuai huko Shehia ya Kizimbani Wilaya ya Magharib “ A” Unguja.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , akiingia ndani ya nyumba ya mkaazi wa shehia ya miwani Bi. Christina John kumfariji juu ya maafa hayo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” akiangalia ukuta uliobomoka kwa mvua wa vyoo vya Skuli ya msingi na sekondari Bwejuu na kuchangia sh.200,000 na gari moja la mawe ili ukuta huo ujengwe haraka ili shule ikifunguliwa wanafunzi wapate huduma ya vyoo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...