Kampuni ya Coco- Cola Kwanza kupitia Maji ya Dasani imedhamini mashindano ya riadha marathon ‘Dasani Marathon’ itakayofanyika Mei 14 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca –Cola Kwanza , Nalaka Hattiachchi , amesema kampuni imedhamini mbio hizo ili kuweza kuchochea riadhaa nchini.

Amesema kuwa wanariadhaa wanaotakiwa kushiriki mbio za Kilomita 10 na 21 na tayari usajili umeanza kufanyika kwa kuwa washiriki 1000.
Rais wa Dar Running Club, Goodluck Elvis amesema mbio hizo zilianza miaka mitatu iliyopita na zimeendelea kwa kuibua wanariadha wengi ambao baadaye wanaweza kuleta historia ya nchi kama ilivyokuwa.

Mshindi wa Dasani Maradho wa kwanza atapata sh. Milioni mbili na wa pili atapata sh.700000 na zawadi mbalimbali zitatolewa na washiriki wanatakiwa kujisajili kwa sh.30000 kulipa kwa M-pesa 243388.
Vituo vya kujiandikisha Colosseum Gym, Masaki,Shoppers Supermarket , Mikocheni na Mlimani City.

Mwanariadha Mkongwe Juma Ikangaa amesema kuwa watu wakiwa tayari kwa kujitoa katika kushiriki riadhaa wanaweza kuwa na rekodi katika dunia.Amesema kinachotakiwa katika ushiriki ni kujiandaa na kuwa na tamaa ya kupata ushindi bila kufanya hivyo riadha itakuwa jina kwa Tanzania.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza , Nalaka Hattiachchi akizungumza na waandishi habari juu ya udhamini kampuni hiyo katika Dasani maradhoni, kushoto ni Rais Dar Running Club , Goodluck Elvis Kulia Mwanariadha Mkongwe , Jumaa Ikangaa.
 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Dasani Marathon inabidi mjipange sana ili msiwe kama wale waandaaji wa marathon iliyofanika tarehe 26/04.
    Mjipange katika waelekezaji wa njia route ili kuepusha wakimbiaji kupotea njia,mkimbiaji akipotea njia inampoteza moyo wa kushiriki.
    Pia mkiweza number za wakimbiaji ziwe za rangi tofauti ili kujua yupi kakimbia ngapi,hii itaweza kuwapa moyo wakimbiaji wapya wakiona hata mtu mnene kakimbia 21KM basi na yeye atafanya juhudi ..fanyieni kazi hayo ili kufanya mbio zenu ziwe nzuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...