Na Mathias Canal, Iringa 

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela amefungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.

Alisema kuwa ili kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini wataalamu wote nchini wanapaswa kubadilishana ujuzi na kushauriana namna ya kuwa na kilimo chenya tija kuliko kuficha ujuzi walionao kwa muktadha wa maeneo husika pekee waliyopo hivyo ni vyema kutumia ujuzi wao kwa makubaliano na maelekezano kwani jambo hilo litachochea zaidi ukuzaji wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Dc Kasesela ameyasema hayo wakati Akizungumza kwenye ufunguzi wa warsha hiyo inayofanyika katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa, warsha inayowahusisha Makatibu Tawala wasaidizi upande wa uchumi kutoka mkoa wa Iringa na Pwani na Maafisa kilimo wa mikoa, Meya wa Manispaa/Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa/wilaya, Wachumi wa Manispaa/Wilaya na Maafisa Kilimo wa Manispaa/Wilaya kutoka Katika Halmashauri za Manispaa na Wilaya kutoka Mkoa wa Pwani na Dar es salaam.

Dc Kasesela ameeleza kuwa Programu hii ya ASDP 2 imeandaliwa baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ASDP 1 iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2006/2007 hadi 2013/201 huku akiwapongeza waandaaji wa warsha hiyo ambao ni OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kutaraji kutekelezwa na wadau mbalimbali kama vile Wizara za sekta ya kilimo, Wahisani, Sekta binafsi, Taasisi zisizo za kiserikali, Wakulima Wafugaji, na Wavuvi.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Meya wa Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni mwenyekiti wa warsha akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...