THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DC SHINYANGA APONGEZA WANANCHI KUJENGA KITUO CHA POLISI ISELAMAGAZIMkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua jengo la kituo cha Polisi kata ya Iselamagazi ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na mbunge wao wa Solwa Ahmed Salimu.

Ukaguzi wa jengo ukiendelea
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akiteta jambo na viongozi wa serikali pamoja na baadhi ya madiwani wa halmashauri kabla ya kuingia kwenye mkutano wa viongozi wa Sungusungu na watendaji wa vijiji,kata na vitongoji kujadili ajenda mbili za ulinzi na usalama pamoja na kuunda ushirika wa vyama vya kuuza mazao ili kuinua wakulima kiuchumi sambamba na kuhifadhi chakula cha akiba ili kukabiliana na janga la njaa hapo baadae.
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akizungumza na viongozi wa Sungusungu,baadhi ya watendaji wa kata ,vijiji,vitongoji na Madiwani wa halmashauri hiyo juu ya kudhibiti uhalifu kwenye tarafa hiyo ya Nindo pamoja na kuwafichua wahalifu ambao huhatarisha hali ya amani.