Halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida zimeagizwa kutenga maeneo yenye hadhi ya kuwa viwanja vya michezo pamoja na kuhakikisha zinakuwa na benki ya wanamichezo katika halmashauri zao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa maagizo hayo leo asubuhi kabla ya kuzindua mashindano ya michezo kwa shule za Sekondari (UMISSETA) kwa ngazi ya mkoa ambapo wanamichezo hao wataunda timu za Mkoa kwa ajili ya mashindano ya kitaifa yatakayofanyika jijini Mwanza mwezi ujao.

Dkt. Nchimbi amesema halmashauri zimekuwa zikiwatelekeza wanamichezo mahiri hivyo wakianzisha benki ya wanamichezo kwa maana ya kuhifadhi kumbukumbu za wana michezo mahiri pamoja na kuwaendeleza hawatapata shida kipindi cha mashindano yoyote. 

Ameongeza kuwa halmashauri zimekuwa zikijisahau katika kuandaa maeneno ya michezo hadi inapofika kipindi cha UMISETA hali inayopelekea kukosekana kwa viwanja vya kufanyia mazoezi ili kuwa na timu bora.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia kabla ya kuzindua mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa wa Singida.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (aliyenyanua ubao) akipiga ubao wa kuashiria uzinduzi wa michezo ya UMISSETA mkoa wa Singida, mbele yake ni wanariadha wakianza mashindano.
 Wanamichezo kutoka Shule za Sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Itigi wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bado napata tabu kwanini viongozi wa nchi hii hukumbuka viwanja vya michezo lakini hawakumbuki maeneo ya kufanyia shughuli za sanaa. Kumbi za michezo ya kuigiza, filamu, muziki. Mwisho shughuli hizi huishia kufanyika baa na kuwanyima haki ya kufurahia snaa hizi watoto. John wa www.theiringa.blogspot.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...