Na Othman Khamks Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Mkusanyiko wa Waumini wa Dini ya Kiislamu katika mfumo wa kushikamana bila ya kufarakana daima huzaa baraka zinazootesha neema na kheir miongoni mwa Umma huo mtukufu mbele ya Muumba wao Mwenyezi Mungu.
Alisema Vitabu vya Dini na  Miongozo yote iliyotolewa katika Vitabu hivyo imekuwa ikielekeza na kusisitiza umuhimu wa Binaadamu hasa Wale walioamini Vitabu hivyo kushikamana pamoja ili lile lengo lao la kumuabudu Mwenyezi Muungu likamilike bila ya kutetereka kwa kitu chochote kile.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa Dua Maalum ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu pamoja na kujiandaa kuukaribishwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaokaribia kuingia wiki chache zijazo dua iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Malindi Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Mamia ya Waumini wa Dini ya Kiislamu, Wananchi pamoja na baadhi ya Viongozi wa Serikali na Kisiasa.
Alisema Waumini na Wananchi wote wanapaswa kuzingatia  umuhimu wa suala la Amani iliyopo Nchini kwani kwa kufanya hivyo kutatoa fursa kwa Waumini hao kutekeleza kwa utulivu Ibada zao sambamba na Wananchi kuendelea na harakati zao za Kimaisha za kila siku.
Akizungumzia ujio la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuingia wiki chache zijazo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitoa wito kwa Wafanyabiashara wote hapa Nchini kuacha tabia ya kupandisha bei za bidhaa muhimu zinazotumiwa kwa wingi na waumini wa Dini ya Kiislamu katika kipindi hicho cha saumu.
Alisema tabia hiyo mbaya ni dhambi kubwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitakuwa na huruma katika kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wowote watakaopandisha bei bidhaa zao bila ya sababu za msingi zitakazokubalika.
Mapema Mufti Mkuu wa Tanzania  Bara Sheikh Abubakar  Zubeir Ali alisema Dua ni fursa kubwa inayompa fursa Mwanaadamu kumuomba Mungu amuelekeze katika njia ya Amani.
Sheikh Zubeir alisema Mwenyezi Muungu muda wote hutarajia kuombwa na waumini wake vyenginevyo anaondosha baraka zake na kutowajaalia kheir na hatma njema waombaji hao anayoisisitiza kila siku kufanywa  na waja wake.
Hata hivyo Mufti Mkuu huyo wa Tanzania alitahadharisha wazi kwamba zipo ishara zinazoanza  kujichomoza za mmong’onyoko wa Maadili unaotishia kutetereka kwa Amani jambo ambalo kila Muumini na Mwananchi anapaswa kuliondoa au kulikemea lisije kuleta athari hapo baadae.
 Waumini wa Dini ya Kiislamu wakisoma Dua maalum ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu pamoja na kujiandaa kuukaribishwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani iliyofanyika katika Msiki wa Ijumaa Malindi Mjini Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akijumuika pamoja na Waumini mbali mbali wa dini ya Kiislamu Nchini katika Dua maalum ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu pamoja na kujiandaa kuukaribishwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kulia ya Balozi  Seif ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Ka’abi pamoja na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam  Sheikha Alhad Mussa Salum.
 Mufti Mkuu wa Tanzania Bara Sheikh Abubakar Zubeir Ali  wa kwanza kutoka Kushoto,  Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud walikuwa miongoni wa  Viongozi walioshiriki Dua hiyo.
 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Madhehebu ya Shia Kutoka Nchni Iran waliojumuipa pamoja na Waumini wa Zanzibar katika Dua ya kuliombea Taifa  Aman.
 Maulamaa na wahadhiri kutoka Nchini Misri nao walikuwa miongoni mwa washiriki wa Dua hiyo iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Malindi.
 Baadhi ya Maimamu wa Misikiti mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi wakisoma Dua hiyo maalum ya kuliombea Taifa Amani na Utulivu pamoja na kujiandaa kuukaribishwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa nasaha ya kuwataka waumini na Wananchi kuendelea kudumisha Amani kwenye Dua ya Kuliombea Taifa amani. Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...