Katika azma yake ya kuhakikisha Watanzania wengi wanapata matangazo yake, Kituo cha Utangazaji cha EFM kimetanua matangazo yake kwa kuongeza masafa ya 91.3 fm Mkoani Mwanza huku Uongozi ukibainisha kuwa matarajio ni kuhakikisha Matangazo hayo yanafika katika mikoa mingine kumi, ikifuatiwa na Mkoa wa Mbeya, Singida, Kilimanjaro, Manyara, Mtwara, Tanga , Kigoma na Dodoma.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa EFM Radio Bwana Denis Ssebo, amesema lengo la kuanza na Mkoa wa Mwanza ni baada ya kuangalia idadi ya watu ambao wanapatikana kupitia Kanda ya Ziwa Victoria lakini pia ukubwa wa jiji hilo baada ya jiji la Dar es salaam.

"Lengo la Efm Radio ni kuhakikisha inahabarisha, inaburudisha, kuwezesha pamoja na kuwapa elimu wasikilizaji wake wote katika kila mkoa itakaposikika. Hivyo mikoa mingine ikae mkao wa kula - tutawafuata mlipo…" amesema Denis Ssebo”, akimalizia na EFM NI KWIKWI!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...