Efm redio imezindua rasmi msimu wa tatu wa mchezo wa sakasaka. Mchezo huu huchezeshwa kila mwaka na mwaka huu utachezeshwa katika wilaya ya Temeke, Kigamboni, Ubungo, Ilala na Bagamoyo. Siku ya leo tarehe 28/05/2017 umezinduliwa rasmi katika kiwanja cha Sinza Tippi wilaya ya Ubungo.

Mchezo huu wa sakasaka huchezeshwa kwa kuficha vitu vyenye thamani ya pesa katika uwanja husika ambapo inampasa msikilizaji afatilie dondoo za kitu hicho pamoja na mahali ili ajue sehemu na aina ya kitu kilichofichwa na atakae kipata atakua mshindi wa pesa taslimu.

Mwaka huu washindi nane katika kila wilaya watajishindia pesa taslimu, ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha shillingi milioni moja akifuatiwa na washindi wa shilingi laki moja na elfu hamsini.
Sehemu ya washiriki wakitafuta vitu vilivyofichwa katika uwanja huo.
Washiriki wa mchezo wa Sakasaka wakisubiri kuhakikiwa vitu walivyoviokota kama ni sahihi.
Meneja matukio Efm redio Neema Mukurasi (wakwanza kulia) akiwa ameshikilia vitu vitatu vilivyo okotwa na mshiriki Mr. Denis Charles (wakwanza kushoto ) vyenye thamani ya shilingi Laki mbili wakiwa na Mtangazaji Denis Rupia (Chogo)
Meneja matukio, uhusiano na mawasiliano Neema Mukurasi akimkabidhi mmoja wa washiriki wa mchezo huo shilingi elfu 50 baada ya kuokota kitu chenye thamani hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...