Na Sultani Kipingo
Emmanuel Macron (pichani) leo ameshinda kwa kishindo kinyang'anyiro cha Urais wa Ufaransa na kumweka kando Marine Le Pen kwenye mbio hizo za kuingia Ikulu ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa, Macron kashinda kwa kupata asilimia 64.78 za kura dhidi ya mpinzani wake Le Pen aliyeambulia asilimia 35.22 za kura. 
Akiwa na umri wa miaka 39, Macron anakuwa kiongozi kijana zaidi kutawala nchi hiyo tangia enzi za utawala wa Napoleon Bonaparte.
"Nimempigia simu Emmanuel Macron usiku huu kumpongeza kwa kushinda kiti cha urais wa Jamhuri ya Ufaransa, " rais anayemaliza muda wake Francois Hollande amesema katika taarifa yake.
Rais Hollande amesema ushindi wa kishindo wa Macron unathibitisha kwamba raia wengi wa Ufaransa wanakubaliana na mustakabali wa Jamhuri hiyo na kuthibitisha uungaji mkono wa Jumuiya ya Ulaya - ambayo Le Pen alikuwa ametangaza kufikiria kujitenga.Mama huyo pia alikuwa anapiga vita sana sera za uraia za Ufaransa ambapo alisema endapo atachaguliwa ataangalia namna ya kuzuia wahamiaji na wakimbizi kukanyaga nchi hiyo.
Marine Le Pen amekubali matokeo na kumpongeza Macron kwa ushindi wake mnono wa kupata asilimia 31 ya kura zaidi ya zake.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...