Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

KATIBU mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi amefunga kozi ya utawala bora iliyoendeshwa na mkufunzi wa FIFA Henry Tandau iliyokuw ainafanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam 

Kozi hiyo inayosimamiwa na Kamati ya Olimpiki ilianza Mei 08 na kufungwa Mei 12 huku kukiwa na washiriki 15 kutoka klabu mbali mbali za ligi kuu na taasisi za michezo. 

Akizungumza wakati wa kufunga kozi hiyo Bayi amesema kuwa hii ni kwa mara ya kwanza kwa wawakilishi kutoka klabu mbalimbali za Ligi Kuu kushiriki katika mafunzo haya ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya michezo nchini. 

Amesema kuwa, ana imani kubwa sana kuwa elimu hii waliyoipata wataenda kuitumia vizuri katika kuziendesha klabu zao na kuzieletea maendeleo kwani msingi mkubwa wa maendeleo ya soka ni kuwa na utawala bora. 

"Elimu hii mliyoipata leo nina imani kubwa sana mtaitumia vizuri kwani wengi wenu mnatoka katika klabu za Simba, Yanga na Azam na maendeleo ya mpira wa miguu yanaletwa na utawala bora na wasiende kuweka vyeti ndani bali wanatakiwa kuvitumia kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo,"amesema Bayi. 

Mkufunzi wa FIFA Henry Tandau amemshukuru Bayi kwa kuweza kukubali kuwa mgeni rasmi kaika mafunzo hayo na kumuahidi kuwa elimu hii waliyoipata wanaimani kuwa washiriki wote wataenda kuelimisha na wengine na kuleta utawala bora kwenye klabu zao. 

Mafunzo hayo ya siku 5 yameratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini huku ikiwa ni kwa mara ya kwanza tofauti na miaka mingine kufanyika mikoani pia yameweza kuleta tija kwa washiriki kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu michezo ikiwemo riadha. 
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akizungumza wakati wa kufunga kozi wa mafunzo ya utawala bora iliyoendesha na Shirikisho la Mpia wa Miguu (FIFA) kupitia kamati ya Olimpiki iliyoanza Mei 08 mpaka Mei 12 Jijini Dar es salaam.
Mkufunzi wa FIFA Henry Tandau akizungumza wakati wa kufunga kozi wa mafunzo ya utawala bora iliyoendesha na Shirikisho la Mpia wa Miguu (FIFA) kupitia kamati ya Olimpiki iliyoanza Mei 08 mpaka Mei 12 Jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi.
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Kituo cha JKM Park Kassim Liogope mafunzo yaliyomaliza leo Jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...