Katika kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel imeendelea kuunganisha huduma yake ya Halopesa na huduma nyingine zaidi ili kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania .

Katika kulifanikisha hilo Halotel imeingia makubaliano ya mkataba wa utoaji wa huduma na kampuni ya Selcom, ushirikiano utakaowawezesha mamilioni ya wateja wa mtandao huo kutoa na kutuma pesa, kununua vocha za muda wa maongezi na kufanya manunuzi mbalimbali.

Hatua hii itawawezesha watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ikiwa ni sehemu ya kufanikisha azma ya serikali ambayo inazitaka taasisi mbalimbali za kifedha kuwafikia wananchi na huduma zao hasa kwa maeneo ya vijijini.

Akizungumza wakati wa makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Bw. Le Van Dai amesema kuwa ni hatua nyingine kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi nchini Tanzania. Sasa kupitia huduma ya Halopesa itakuwa imewezesha kupanua wigo kwa wateja wa mtandao huo kuweza, kutoa na kuweka fedha, pamoja na kufanya malipo mbalimbali kwa urahisi zaidi.

“Ushirikiano huu ni wa kipekee katika kurahisisha maisha ya watanzania ambao wamekuwa wakipata tabu kupata huduma za kifedha kutokana na maeneo wanayoishi. Sisi kama Halotel hadi sasa tumewafikia watanzania kwa zaidi ya asilimia 95. Hivyo ni dhahiri kwamba wateja watakaojiunga nasi wataweza kutoa au kuweka fedha huko huko waliko kupitia kwa mawakala wetu ambao wameenea nchi nzima,” alisema Dai. 
  Mkuu wa Halotel, Le Van Dai (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango wa Selcom, Benjamin Mpamo wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kibiashara baina ya kampuni hizi yatakayo wawezesha wateja wa  Halopesa kutoa na kuweka pesa, pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia mawakala wa Selcom nchi nzima.

  Mkuu wa Halotel, Le Van Dai (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango wa Selcom, Benjamin Mpamo wakitia saini mikataba ya makubaliano ya kibiashara baina ya kampuni hizi yatakayo wawezesha wateja wa  Halopesa kutoa na kuweka pesa, pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia mawakala wa Selcom nchi nzima, Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa kampuni hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...