Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

HOSPITALI ya Wilaya ya Mkuranga imepata msaada wa wodi ya wazazi vyenye thamani ya sh. Milioni 65 kutoka kwaTaasisi ya Dhi Nureyn .

Akizungumza baada ya makabidhiano ya vifaa wodi ya wazazi , Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega amesema kuwa wodi ya wazazi katika hospitali hiyo ilikuwa na hali mbaya kwa kukosa vitu muhimu ambavyo vinasababisha kupoteza maisha kwa mama au mtoto .

Amesema kuwa kutokana na wanawake wa Wilaya walikuwa hawana uhakika katika masuala ya uzazi lakini sasa suluhisho limepatikana kwa taasisi hiyo kutoa vitu hivyo katika kuokoa maisha ya mama na mtoto katika hospitali hiyo .

Ulega amesema kuwa kutokana tatizo hilo aliamua kwenda kuomba katika taasisi ya Dhi-Nureyn ambao waliangalia mahitaji katika wodi ya wazazi na kuamua kutoa msaada huo licha kuwa na changamoto zingine katika hospitali ya Mkuranga .

Nae Mwenyekiti wa taasisi ya Dhi-Nureyn , Sheikh Said Abri amesema kuwa baada ya kupata maombi kutoka kwa Mbunge wa Mkuranga ,Abdallah Ulega juu ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga hasa katika kuokoa maisha mama na mtoto tuliona jambo la msingi kutekeleza.

Amesema kuwa wataendelea kuwa kusaidia kadri ya uwezo unapopatikana ili hospitali hiyo kuendelea kutoa huduma bora kwa kuwa na vifaa vinavyostahili katika kuhudumia wananchi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkuranga, Steven Mwandambo amesema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati mwafaka kutokana na vifaa hivyo kukosekana kwa muda mrefu huku mipango ilikuwa ikifanyika.
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga wakikabidhiwa vifaa vya Wodi ya wazazi kutoka kwa watendaji wa Taasisi ya Dhi-Nureyn katika Hafla ilyofanyika Mkuranga.
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga wakikabidhiwa vifaa vya Wodi ya wazazi kutoka kwa watendaji wa Taasisi ya Dhi-Nureyn katika Hafla ilyofanyika Mkuranga.
.

 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega Akizungumza na wananchi wakati wa makabidhibiano ya vifaa katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Mkuranga leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi-Nureyn,Shekh Said Abri akizungumza juu msaada huo waliotoa katika hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.Picha na Chalila Kibuda-Globu ya Jamii Mkuranga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...