Mkulima
Christopher Nduva (kushoto) kwa furaha akipokea maelezo yaliyopo kwenye
kipeperushi cha mahindi cha Yara Tanzania kutoka kwa Afisa Ugani (bwana shamba) wa Yara Tanzania, Andrew Mwangomile (pili kulia) baada ya zao lake kugundulika changamoto
inayolikabilia. Kulia ni muhusika mkuu wa duka la pembejeo Bw. Antony
Kalenga ambapo huduma ya zahanani ya mimea ilitolewa.
Wakulima
wamiminika kwenye duka dogo la pembejeo lilipo Mafinga kwa ajili ya
kupeleka mazao yao kwa ajili ya kupata utatuzi. Bwana shamba wa kampuni
ya Yara Tanzania Ltd, Andrew Mwangomile aliwaelezea wakulima walioleta
mahindi yao kwa ajili ya kupatia ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba.
Bwana
shamba huyo alipohojiwa aliesema, Yara Tanzania imeandaa huduma maalumu
inayoitwa "crop clinic day" (siku ya zahanati ya mimea) huduma hii
inafanana na ile ya binadamu au kiumbe hai yeyote anapohitaji huduma ya
kwanza akijisikia kuumwa ili kupata huduma ya kwanza. Kwenye siku hii
maalumu wakulima huleta mizizi, majani au zao lenyewe kwa ajali ya bwana
shamba kuweza kumsaidia kutatua kwa haraka tatizo linalokabili mmea
huo."
Moja
ya kauli mbiu zetu ni mkulima afanikiwe na kuweza kulisha dunia kwa
kutoa huduma muhimu zinazoweza kumsaidia mkulima kuzalisha mazao bora na
sio bora mazao. Yara Tanzania inahakikisha ili mpango huo utekelezeke
ni kusaida wakulima kutatua changamoto mbali mbali ya mazao. Siku ya
zahanati kwetu ni muhimu na tunatoa huduma hii Bure kwenye mikoa yote
nchini kushikiana na mawakala wadogo na wakubwa. Aliongeza alipohojiwa
kwa njia ya simu afisa masoko na mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Linda
Byaba.
Afisa
Ugani (bwana shamba) wa Yara Tanzania, Andrew Mwangomile akiwaelezea
wakulima waliotembelea kwenye duka la pembejeo lengo la Zahanati ya
mimea iliyoanzishwa na Yara Tanzania kwa kutumia mfano wa zao la mahind.
Afisa Ugani (bwana shamba) wa Yara Tanzania, Andrew Mwangomile akielezea aina ya virutubisho vinavuohitajika kwenye zao la mahindi na vinavyopatikana kwenye mbolea aina ya YaraMila CEREAL.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...